Kamanda wa poilisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile kushoto
akitoa msimamo mkali kwa jeshi hilo wakati akiongea na wamiliki na waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda
wa Manispaa ya Morogoro katika mkutano wenye lengo la kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na ajali za pikipiki vinavyodaiwa vingi vinatokana na kutozingatia sheria za usalama barabarani ambazo zinasababisha vifo na wengine kupata vilema kulia ni Mkuu wa
Usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Leornad Gyndo.
Kamanda Shilogile akipitia kalatasi yenye mapendekezo kutoka kwa bodaboda katika mkutano huo, kulia ni RTO, Leornad Gyndo.
Mmoja wa bodaboda akizungumza jambo katika mkutano huo huku viongozi wa bodaboda wa kwanza kushoto na pili wake nao wakifuatialia mazungunzo ya mkutano huo.
Hapa sehemu ya bodaboda wakimsikiliza kamanda wa wa polisi wakati akiongea.
Mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda naye akitokea kero wanazozipata kutoka kwa askari wa usalama barabarani na wale wa voda faster katika mkutano wenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani na namna ya kuzingatia sheria zake ili kuweza kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na marejeru ambapo kuanzia januari hadi juu jumla wa waendesha pikipiki Manispaa ya Morogoro wameripotiwa kufariki dunia kwa ajali za pikipiki na wengine kujeruhiwa vibaya.
Mmoja wa Bodaboda akiwa amempakia mwenzake juu ya kiroba huku akiwa hana kofia ngumu (ELMENT)ikiwa mojawapo ya makosa ya usalama barabarani wakati wakisafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika kata ya Doma wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment