BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MRADI WA SIMLESA WATOA MBINU MBADA YA KUKABILIANA NA HALI YA HEWA KATIKA KILIMO TANZANIA.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Anthony Mtaka kushoto akimsikiliza Mratibu Msaidizi wa taasisi ya serikali inayojishughulisha na mradi wa mifumo ya kilimo endelevu ya mahindi na mikunde mashariki na kusini na kusini mwa afrika nchini (SIMLESA) Bashiri Mkoko (katikati) akieleza jambo wakati wa maonyesho ya kilimo cha mseto na shamba darasa unaofadhiliwa na nchi ya Australia zikihusisha na nchi tano za Afrika ikiwemo Kenya, Ethiopia, Tanzania, Malawi na Msumbiji.

Katika utafiti huo imelenga katika kulima mazao mchanganyiko ya mahindi na Mikunde kwa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na kuvumilia ukame ili kuweza kuongeza uzalishaji wa mazao katika ngazi ya kaya hapa nchini ambapo mashamba ya mfano yapo katika kijiji cha Vitonga kata ya Mlali wilayani humo na kulia ni Mtafiti Kiongozi wa taasisi hiyo, George Iranga. 
Mkulima wa kijiji cha Vitonga kata ya Mlali kushoto akieleza jambo kwa Mkuu wa ya Mvomero mkoani Morogoro, Anthony Mtaka kulia wakati wa maonyesho ya kilimo cha mseto na shamba darasa katika mashamba ya mfano ya mkulima huyo kijijini hapo.

 Baadhi ya wataalamu wa kilimo ngazi ya wilaya ya Mvomero wakiangalia mazao ya Alizeti kwa moja ya mashamba ya mfano ya zao hilo baada ya mbegu zake kufanyiwa utafiti kupitia mradi huo
 Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro Anthony Mtaka akizungumza na wanakijiji cha vitonga kata ya Mlali katika wilaya hiyo juu ya umuhimu wa kulima kilimo cha mseto na kutumia mbegu bora zinazovumilia ukame baada ya kukagua maonyesho ya kilimo mseto na shamba dasara kupitia mradi wa mifumo ya kilimo endelevu ya mahindi na mikunde mashariki na kusini na kusini mwa afrika  (SIMLESA),

Katika mradi huo unafadhiliwa na nchi ya Australia kwa nchi tano za Afrika za Malawi, Msumbiji, Kenya, Ethiopia na Tanzania ambapo utafiti huo ina lenga katika kumuinua mkulima katika uchumi kwa kulima mazao mchanganyiko ya mahindi na Mikunde kwa ajili ya kuongeza uzalishaji ngazi ya kaya mkoani hapa, kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Mlali Juma Abdallah na kulia ni Mtafiti kiongozi wa taasisi ya Simlesa, George Iranga na Kaimu mratibu wa taasisi hiyo, Bashir Makoko.
Picha na Abdallah Chilemba. 
 Baadhi ya wanakijiji cha Vitonga wakimsikiliza kuu wa wilaya hiyo Anthony Mtaka katika mkutano huo.


Na ESTHER MWIMBULA MVOMERO.

WATAFITI wa Miradi mbalimbali nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa tafiti na miradi ya kilimo wanayoibuni inakizi tija kwa wananchi katika kukuza uzalishaji wa mazao ili kuweza kukuza uchumi na maendeleo katika ngazi za kaya kijiji na hatimaye taifa kwa ujumla itakayosaidia kuondokana na umasikini.

MKUU wa wilaya ya Mvomero iliyopo Mkoani Morogoro Antony Mtaka amesema hayo alipokuwa akikagua shamba darasa la kilimo mseto katika kijiji cha vitonga kata Mlali tarafa ya Mlali Wilayani Mvomero ufadhiri wa Australia na kuzihusisha nchi za Kenya,Ethiopia,Tanzania,Malawi na Msumbiji ambapo tafiti hiyo imelenga katika kulima mazao mchanganyiko ya mahindi na Mikunde kwaajili ya kuongeza uzalishaji ngazi ya kaya.

Mtaka alisema kuwa watafiti nchini wanatakiwa kuhakikisha tafiti zao zinawanufaisha wananchi kwaajili ya kuwaletea maendeleo na kuwapunguzia umasikini kupitia sekta ya kilimo na kuachana na tabia ya kuendesha tafiti zinazojali maslai yao binafsi.

Wito huo umekuja mara baada ya mkuu wa wilaya hiyo kutembelea kutembelea mradi wa kilimo mseto kilicho anzinshwa na asasi isiyo kuwa ya kiserikali ya Simlesa ambayo inajishughulisha na kilimo mseto cha mahindi na mkunde ambayo inafadhiliwa na serikali ya Ausralia.

Alisema kuwa watafiti wengi wamekuwa wakijinufaisha wenyewe bila kujali mahitaji ya wananchi kwa kuanzisha miradi isiyo na tija kwa jamii ambao ndiyo walekwa wakuu wa tafiti mbalimbali za kilimo ambapo kufanya hivyo kunarudisha nyuma maendeleo wa wananchi na kuwaacha katika hali ngumu ya kiuchumi na kuwa tegemezi kwa viongozi wa serikali za vijiji vyao.

Alisema kuwa mradi wa kilimo mseto cha mahindi na mikunde ni mradi ambao umeonesha mafanikio katika kijiji hicho kutokana na wakulima wengi wa kijiji hicho walikuwa wakitegemea kilimo cha aina moja ambapo walikuwa wana shindwa kuendana na mabadiliko ya hari ya hewa.

Hivyo aliwataka wakulima hao kuendelea kulima kilimo hicho kwani kitawakwamua na janga la njaa ambalo limekuwa likiwakumba wakulima wengi ambao hawafati sheria na taratibu za kulima mazao mbalimbali na badala yake kutegemea zao moja ambalo la mahindi pekee .

Naye kaimu mratibu wa mradi huo Bashir Makoko alisema kuwa mradi huo ulianzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kuwaelimisha wakulima kulima kilimo cha aina hiyo ambayo itawafanya wapate chakula cha kutosha na kuondokana na janga la njaa ambalo lina wakumba wakulima wengi ambao hawajui jinsi ya kulima na kuendana na mabadiliko ya hari ya hewa .

Makoko alisema lengo la mradi huo ni kuwawezesha wakulima kuongeza uhakika wa chakula ,kipato na uchumi kwa kutumia kilimo cha mseto cha mahindi na mikunde ndani ya kilimo hifadhi , na wakulima hao kutambua kilimo kinacho endana na mabadiliko tya hari ya hewa .

Hivyo aliwaomba wakulima hao kuendelea kulima kilimo hicho na kutoa elimu kwa wakulima wengine ili waweze kulima mazao ya kutosha na kujikwamua kimaisha na walime kwa kujipatia kipato kwa manufa ya familia zao na taifa kwa ujumla.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: