Moja ya familia za Sokwe.
Ruhondeza
alikuwa baba wa familia ya sokwe iitwayo Mubare ambayo imekuwa
ikuwavutia watalii kuanzia miaka ya tisini.
Lakini kwa nini akaitwa
Ruhondeza? msemaji wa shirika la wanyama pori nchini Uganda Lilian
Nsubuga jina la sokwe huyo liliashiria tabia yake.
Alikuwa mzembe sana
na alipenda kulala sana.
Ruhondeza ni jina ambalo linamaanisha mtu
anayependa kulala na linatokana na lugha ya kabila la Bafumbira nchini
Uganda.
Ingawa Ruhondeza alikuwa na tabia ya kuzembea zembea na
kujivuta vuta, upande wa wanawake hakuzembea hata kidogo.
Bi Nsubuga
anasema aliwakasirikia sana wanaume wa familia yake walipojaribu
kuwatongoza wanawake wake.
Alikuwa mkali sana kiasi kwamba kwa wakati
mmoja hakuwa na mrithi kwa sababu wanaume wengi wa familia yake
walitoroka kuukwepa ukali wake.
Kwenye ulimwengu wa sokwe, wanawake wote
ni wa sokwe anayeiongoza familia.
Siku za mwisho za Ruhondeza zilijaa upweke ingawa haijulikani
aliwazaa watoto wangapi na kinachojulikana ni kwamba aliwazaa watoto wengi
lakini wakati wa kufa kwake alikuwa peke yake.
Mwanzoni mwa mwaka huu familia ya sokwe mwengine aitwaye Mubare
ilivaamia na sokwe wengine wa msituni na kwenye harakati za kupigana
baadhi ya sokwe walitoroka kuyanusuru maisha yao.
Kijana mmoja wa
Ruhondeza aitwaye Kanyonyi aliweza kuwaokoa jamaa saba wa familia yao na
kutoroka nao na wale wengine hawajulikani walipo.
Baada ya vita hivyo
Ruhondeza alijipata akiwa peke yake na hakuungana tena na familia yake.
Madaktari wa wanyama pori wanaufanyia uchunguzi mwili wa Ruhondeza
ili kuthibitisha kilichokisababisha kifo chake na ripoti ya kwanza ambayo
imetolewa sasa inasema kifo chake kilisababishwa na uzee.
Maiti yake haikuwa na majeraha yoyote na meno yake yalikuwa
yameharibika kabisa na wakati wa kifo chake hakuweza kula vizuri huku mwili
wake ulikuwa umedhoofika kabisa na misuli yake kulegea legea.
Ruhondeza
alizikwa Juni 27 na sanamu ya ukumbusho yake itajengwa mahali alipozikwa
Ruhondeza ili iwe ukumbusho wa maisha yake na mchango wake wa kuanzisha
utalii wa sokwe nchini Uganda.
0 comments:
Post a Comment