JOPO ZIMA LA BLOG YENU INAWATAKIWA WAUMINI WOTE WA DINI YA KIISLAM NCHINI NA DUNIANI KWA UJUMLA KUFUATA MATENDO MEMA YALIYOAMSHISHWA NA MWENENYEZI MUNGU KATIKA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NA KUAHCA MATENDO AMBAYO YATAHARIBU FUNGA ZETU IKIWA NI MOJA YA NGUZO KUU YA DINI YA KIISLAM.
TUNAWATAKIA FUNGA NJEMA, AMINA.
MAELEZO MUHIMU YA KUYAFAHAMU WAKATI WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.
ALLAH Subhaanahu wa Ta’ala) alipanga kuwa mwaka uwe na miezi kumi na
mbili, na katika hiyo akaichagua baadhi akaitukuza na kuifadhilisha zaidi ya
mengine.
Mwenyezi Mungu anasema:
“Hakika idadi ya miezi mbele ya Allah
ni miezi kumi na mbili kati ya hiyo mna minne iliyo mitukufu."
Nayo ni Dhulqaada, Dhulhijja, Muharram,
na Rajab.
Baada ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) kuifadhilisha miezi
hii minne akaufadhilisha vile vile zaidi kuliko hata miezi hii minne mwezi
tuliyo ndani yake nao ni mwezi wa Ramadhani usiku wa cheo (Laylatul Qadr)
katika mwezi huu tokeo kubwa ni kuteremshwa kwa Qurani.
Kwa ilivyokuwa mwezi huu ndio bora wa
miezi yote, hivyo basi mema yafanywayo ndani yake yanakuwa ni bora na yanalipwa
ziada kuliko miezi mengine. Hivyo basi inatakiwa kwa muislam kujibidiisha
katika kufanya mema na kuepuka mabaya
hasa awapo katika mwezi huu mtukufu. Baadhi ya mambo tutakiwayo kuyatekeleza.
vKusoma
Qurani
Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)
“Mwezi wa Ramadhani ambayo
imeteremshwa ndani yake Qur-an hali ya kuwa ni uongofu kwa watu …………"
Kwa kuwa katika mwezi huu ndio Qurani
iliteremshwa kwa Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam), inatakiwa kwa muislam kufanya bidii kuisoma
angalau juzuu moja kwa siku ili aweze kumaliza msahafu ifikapo mwisho wa mwezi
huu wa Ramadhan.
vKuharakisha
kufungua.
Miongoni mwa sunna tukufu zinazotakiwa
kwa mfungaji katika mwezi huu kuzikimbilia, ni kuharakisha kufungua baada tu ya
kuzama jua, kwani Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema katika hadithi iliopokewa na Tirmidhy,
Ibnu khuzayma na Ibnu Habban, amesema Bwana Mtume Muhammad (Swallah Llahu alayhi
wa sallam).
“Hakika nimpendaye zaidi miongoni mwa
waja wangu ni anayefanya haraka katika wao kufungua saumu.”
vKusali
usiku.
Inatakiwa kwa muislam kuyatumia masiku
ya mwezi huu mtukufu katika kumuabudu Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kusali na kufanya ibada
nyengine, kwani ni mwezi wa pekee ambao ndani yake kunapatikana usiku wa cheo (Laylatul
Qadr) ambao ibada ya usiku huo inalingana na ibada ya miezi elfu moja, na kwa
hekima yake Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) hakutubainishia kuwa ni usiku wa tarehe ngapi.
Na hii
ni moja miongoni mwa fadhila za kusali katika masiku ya mwezi huu. Vile vile
mwenye kusimama kwa ibada katika masiku haya husamehewa makosa yake yote
yaliotangulia,
kama alivyosema Bwana Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam):
“Mwenye kusimama usiku wa Ramadhani
kwa kufanya ibada hali ya kuwa na imani na kutaraji thawabu anasamehewa
yoteyaliotangulia miongoni mwa makosa yake.”
(Bukhari na Muslim).
Kula daku vile vile ni miongoni mwa sunna
tukufu zinazodharauliwa na wengi kati ya waislam na fadhila zake ni kubwa
kupita kiasi, miongoni mwazo ni kurehemewa na Allah na kutakiwa msamaha na
malaika watukufu kama alivyosema Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) katika hadithi.
“Hakika Allah na Malaika wake
wanawarehemu wenye kula daku.”
(Twabrani, Ibnu Habban).
Vile vile Bwana Mtume (Swallah Llahu
alayhi wa sallam) amesisitiza katika hadithi kwa kusema kuwa:
“Hakika daku ni baraka amekupeni
Allah, hivyo basi musiiache”.
(Annasai)
vKukaa
Itikaaf.
Inatakiwa kwa muislam kuujaalia mwezi
huu na kuutumia katika kuchuma na kuvuna aina tofauti ya mema ikiwemo Itikaaf,
kwani ni miongoni mwa ibada bora sana zinazomkurubisha mja kwa Mola wake (Subhaanahu wa Ta’ala) hasa awapo katika mwezi huu
wa Ramadhani, kwani baadhi ya wanavyuoni wamesema kuwa haisihi ibada hii ya
itikaaf pasi na funga.
Na yatoshe malipo makubwa yaliotajwa katika hadithi;
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema;
“Mwenye kukaa itikaaf siku kumi katika
mwezi wa Ramadhani, basi ni
kama aliyehiji na akafanya umra mara mbili mbili."
(Bayhaq)
vkutoa sadaka.
Miongoni mwa ibada tukufu alizokuwa
akizifanya Bwana Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni kutoa sadaka na alilipa umuhimu
sana jambo hili hadi
wakati wa kuondoka kwake ulimwenguni alipokuwa katika sakaratul mauti kila
alipopata fahamu ilikuwa akimuuliza Bibi Aisha (‘Alayhis Salaam) iwapo ashazitoa
sadaka zile dirhamu nne zilizokuwa
nyumbani? Kadhalika kutoa huku kwake kulikuwa kukiongezeka katika Ramadhani.
vKumtaja
Allah (Subhaanahu wa Ta’ala.
Katika mwezi huu wa Ramadhani kadhalika inatakiwa kwa muislam
kuwa mengi ya maneno yake yawe katika kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), kwani ni jambo
ambalo linasaidia katika kuusafisha moyo wake na kuiboresha funga yake.
Allah (Subhaanahu
wa Ta’ala) ametuamrisha tumtaje kwa wingi katika aya nyingi za Qurani, na hii ndio
ibada pekee aliyosema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) kuwa ifanywe kwa wingi, na miongoni mwa aya
hizo.
“Enyi Mlioamini mtajeni Allah kwa
wingi na mumtakase yeye asubuhi na jioni.”
(Al- Ahzaab 41 na 42).
Kadhalika Mtume (Swallah Llahu alayhi
wa sallam) alitufundisha
aina tofauti za kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ili tusichoke na jambo hili kwani mwanadamu
ni mwepesi wa kuchoka na jambo moja tu. Vile vile akatuonyesha tofauti kubwa
iliopo kati ya anayemtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na asiyefanya hivyo kati hadithi aliposema;
“Mfano wa anayemtaja Allah na asiyemtaja ni mfano wa mtu aliyehai na aliyekufa.”
(Bukhari).
Haya ni baadhi ya yanayotakiwa kufanywa na
muislam, hasa awapo ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivyo basi tujihimu
katika kuyatekeleza haya tuliyoelezwa na tumuombe Allah atutakabaliye matendo
yetu “Amin”.
0 comments:
Post a Comment