Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika fainani
hiyo,Mh. Said Meck Sadick (mwenye suti katikati) akiwa pamoja na
wachezaji wa Timu ya Yanga wakati akiwakabindi Kombe la ubingwa wa
Cecafa Kagame Cup 2012
Wachezaji wa Yanga wakilizungusha Kombe hilo kwa mashabiki wao waliofurika kwa wingi uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. m
Viongozi na wachezaji wa yanga wakishangilia sambamba na kombe.
Mfungaji wa goli la kwanza dhidi ya Timu ya Azam,Hamis Kiiza akiwa na kombe hilo mbele ya Mashabiki wa Yanga.
Sehemu ya mashabiki wa klabu ya Yanga wakishangilia ushindi huo.
KLABU ya Yanga Afrika ya Dar es Salaam nchini Tanzania
imefanikiwa kutea ubingwa wake na kutwaa kombe la Kagame kwa mara ya
pili mfululizo baada ya kuipa kichapo cha magoli 2 -0 timu ya soka ya
Azam FC katika mchezo wa fainali ambayo imeshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza.
Katika mchezo huo Yanga ambao hawakuanza vizuri mchezo huo hapo jana
na kuruhusu mashambulizi kutoka kwa wapinzani wao wakionekana kupania zaidi kupata ushindi.
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Hamis Kiiza ndiye aliyeweza kufufua matumani kwa Yanga baada ya kupenya ngome ya Azam na kuvumania nyavu katika dakika ya 44 ya kipindi cha
kwanza na kufunga bao la kuongoza.
Kama hiyo haitoshi vijana hao wa kocha mpya wa mabingwa hao,Tom Saintfietkutoka nchini Ubelgiji walijipanga vema na kuonesha
mashambulizi na hatimaye katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza
katika kipindi cha pili mchezaji, Said Bahanuzi (Side Boy) aliongeza bao la pili.
Kwa matokeo hayo Yanga sasa imetawazwa rasmi kuwa mshindi wa kombe la
Kagame na kufikisha rekodi ya mara tano ya kutwaa kombe hilo ambapo
walitwaa kombe hilo mwaka 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.
0 comments:
Post a Comment