Mtendaji mkuu wa mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere, Joseph Bujiku kulia akionyesha kitabu kiitwacho "INSHA ZA MAPAMBANO YA WANYONGE" mara baada ya kuzindua katika mkutano mkuu wa 17 wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) juu ya kuandaa maoni ya wakulima wadogo ya kuwasilisha kwa tume ya inayoratibu mchakato wa katiba wa maoni ya katiba mpya katika warsha iliwakutanisha wakulima wa Tanzania bara na Visiwani mkoani Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji (MVIWATA) Stephen Ruvuga.
Mr Joseph Bujiku kulia akisaidiwa na Mtunza Hazina Mviwata taifa, Ester Malya kushoto na katikati ni Stephen Ruvuga.
Mr Bujiku akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Mtendaji mkuu wa mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere Joseph Bujiku akizungumza jambo katika mkutano, kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA)Stephen Ruvuga.
Mwenyekiti Jukwaa la katiba Tanzania Deus Kibamba akifafanua jambo huku Mtendaji mkuu wa mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere Joseph Bujiku kulia na Mkurugenzi Mtendaji wa (MVIWATA) Tanzania, Stephen Ruvuga wakati akizungumzia juu ya mfumo wa katiba katika mkutano huo.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo kutoka Tanzania bara na Visiwani wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa ufunguzi katika hoteli ya Glonency Nane Nane Morogoro.
0 comments:
Post a Comment