BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DC AMANZI AWATAKA WANANCHI WANAOZUNGU​KA VYANZO VYA MAJI NA MILIMA ULUGURU KUACHA TABIA YA KUCHOMA MOTO KWA LENGO LA KUWINDA WANYAMA JAMII YA NDEZI KWA AJILI YA KITOWEO MOROGORO.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tisa ya kuwajengea uwezo viongozi na wananchama hao, kulia ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kikundi Sheria Ally na kushoto ni Mwenyekiti wa shirika la lisilo la kiserikali la Tushikamane, Ununu Mng’oo.
 Mjumbe wa mkoa wa Morogoro katika baraza la Asasi za kiraia Tanzania (AZAKI) Angelus Runji kulia akifafanua jambo kwa viongozi na wananchama wa shirika la lisilo la kiserikali la Tushikamane.
 Mratibu wa fedha na manunuzi katika muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro, Elizabeth Priscus kulia akitoa mafunzo ya namna ya usimamizi wa fedha na udhibiti wa fedha katika mafunzo hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi akikabidhiwa zawadi ya kuku jogoo na Aziza Ramadhan ambaye ni Mratibu maendeleo ya jamii na watoto katika shirika lisilo la kiserikali la Tushikamane mara baada ya mkuu huyu kufungua mafunzo hayo katikati ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kikundi Sheria Ally.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi akimsalimia na mmoja wa wanachama wa shirika hilo, Hamisa Rajabu mara baada ya kuwasili katika ofisi za shirika.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi wa pili kutoka kulia akipata maelezo kutoka kwa Mjumbe wa mkoa wa Morogoro katika baraza la Asasi za kiraia Tanzania (AZAKI) Angelus Runji wa kwanza kushoto wakati msafara wa mkuu huyu ukielekea katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tisa ya kuwajengea uwezo viongozi na wananchama wa shirika hilo yanayofanyika katika shule ya msingi ya kijiji hicho kilichopo katika kata ya Kiroka wilaya ya Morogoro Vijijini mkoani hapa. kutoka kulia ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kikundi Sheria Ally na wapili ni Mratibu wa fedha na manunuzi katika muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro, Elizabeth Priscus.

MKUU wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi amewataka wananchi wanaozunguka vyanzo vya maji na milima ya Uluguru kuacha tabia ya kuchoma moto kwa lengo la kurahisisha uwindaji wa wanyama aina ya ndezi wanachotumia kama kitoweo kwani kwa kufanya hivyo kumekuwa kukisababisha uharibifu wa mazingira mkoani hapa.

Akizungumza na viongozi na wananchama wa shirika lisilo la kiserikali la Tushikamane wakati wa ufunguzi wa mafunzo wa kuwajengea uwezo, Amanzi alisema kuwa sio vitendo vizuri kwa baadhi ya wananchi kuchoma moto misitu kwa lengo la kurahisisha namna ya uwindaji na kuwataka kutumia njia nyingine za uwindaji ikiwemo kutega mitego ya nyavu ili kuepuka uharibifu wa mazingira.

Amanzi alisema kuwa kwa kipindi hiki ambacho nchi mbalimbali duniani zimekuwa zikikaribiana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi hivyo ipo haja kwa wananchi wanaoshi katika vijiji vilivyo karibu na vyanzo vya maji na milima kubadili tabia na kulinda maeneo hayo ili kuepuka athari ambazo vinaweza kujitokeza siku za baadaye.

“Sioni sabau ya wawindaji kutumia mwanya huu kuchoma nyasi eti kwa kisingizio cha kuhalarisha upatikanaji wa ndezi wakati huu wa kiangazi dhana hii jamani tuachane nayo na badala yake tuwatega ndezi hao kama kipindi cha masika ili kuepuka athari ambazo zinaweza kujitokeza katika siku za baadaye” alisema Amanzi.

Amanzi alisema kuwa mbinu ambayo wawindaji wamekuwa wakiitumia nyakati za masika kuwanasa ndezi itumiwe hiyo hiyo ili kuepusha athari za uharibifu wa mazingira na kuwa kitendo cha kuchoma nyasi moto kipindi cha kiangazi kimekuwa kikisababisha uharibifu mkubwa ndani ya jamii ikiwemo kupungua kwa mvua, kuharibu vyanzo vya maji na kuteketeza viumbi hai.

Naye Mwenyekiti wa shirikala hilo la Tushikamane lenye makazi yake makuu katika kijiji cha Kikundi kata ya Kiroka wilaya ya Morogoro vijijini, Ununu Mng’oo alisema kuwa lengo la kuanzisha shirika hilo ni kutoa elimu katika sekta mbalimbali ndani ya jamii inayowazunguka hapa nchini.

Mng’oo alisema kuwa sekta hizo ni pamoja na elimu, afya, kilimo na mifugo, mazingira na maendeleo ya jamii na watoto ambapo kwa sasa wameanza na kujikita katika kutoa elimu juu ya namna ya utunzaji wa vyanzo vya maji na milima ya uluguru.

“Shirika letu kwa sasa tumejikita katika suala zima la kutoa elimu kwa wananchi ya namna ya kutunza vyanzo vya maji na mazingira hasa katika mito yetu ya kudumu ukiwemo Mgoe na Nyasule ambapo vyanzo vyote vya mito hiyo ikitokea katika mlima Kungwe na hili ndilo tatizo kubwa lililopo katika vijiji vinavyopita mito hiyo kwani kumekuwa na uharibifu mkubwa wa kuharibu kwa mazingira” alisema Mng’oo.

Katika mafunzo hayo ambayo yanahusisha viongozi na wananchama wa shirika hilo wapatao 34 yatafanyika kwa siku tisa kwa nyakati tofauti ndani ya miezi mitatu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: