DK KAFUMU AKIWA MWENYE FURAHA MARA BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA IGUNGA.
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya
Tabora imetengua matokeo ya Ubunge wa Mbunge wa jimbo la Igunga Mh. Dalaly
Peter Kafumu ambaye alichukua nafasi hiyo baada ya mbunge wa zamani wa jimbo
hilo Rostam Azizi Kujiuzulu.
Mahakama imemvua Ubunge Dk.
Kafumu hii leo katika Hukumu ya kesi ya Kupinga matokeo ilifunguliwa na
aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Chadema, Joseph Kashindye dhidi ya Dk Kafumu,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.
Mbali na Dk Kafumu, washitakiwa
wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa
Uchaguzi huo, Protace Magayane. Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi Machi 26
na Jaji Mary Shangali.
Zaidi ya malalamiko 13
yaliwasilishwa katika Mahakama hiyo.
0 comments:
Post a Comment