BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAMASHA LA MICHEZO LA IDD EL FITRI YALETA MSISIMKO MOROGORO.

Mshambuliaji wa timu ya soka ya taasisi ya The Islamic Foundation Tanzania, Said Haji ambaye ni mpiga picha kituo cha TV Imani kushoto akitafuta namna ya kumtoka mchezaji wa timu ya Bagamoyo, Saidi Salum kulia huku Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Aref Nahd akiangalia ili kutoa msaada wakati wa mchezo wa soka katika tamasha la Idd El Fitri lililofanyika kwenye uwanja wa chuo kikuu cha waislam (MUM) Morogoro ambapo katika mchezo huo Bagamoyo ilishinda bao 1-0.
WAUMINI wa dini ya kiislam wameadhimisha sikukuu ya Idd El Fitri kwa kufanya tamasha la michezo aina mbalimbali kwa kushirikisha wanamichezo kutoka mikoa mitatu iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro.

Wanamichezo hao ambao wameshiriki michezo hiyo ni kutoka Jiji la Dar es Salaam, Pwani na wenyeji Morogoro wakishindana katika michezo ya mpira wa miguu, mbio za baiskeli ya magurudumu mawili na matatu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika viwanja vya chuo hicho Mwenyekiti wa taasisi ya kiislam ya Islamic Foundation, Aref Nahd alisema kuwa zaidi ya michezo mitatu ilishindaniwa kwa wanamichezo kushindana katika michezo ya soka wanaume, mbio za baiskeli magurudumu mawili na matatu walemavu.
Nahd alisema kuwa lengo kuu la tamasha hilo ni kuwakutanisha waumini wa dini ya kiislam kusherhekea sikukuu ya Idd El fitri kwa kucheza michezo aina mbalimbali ambapo katika mchezo wa soka timu ya kituo cha Redio Iman na Luninga iliyokubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa vijana wa Bagamoyo ambapo bao pekee la washindi hao lilipachikwa na Idd Kiboksi.

Katika mchezo wa pili Wami-Dakawa waliitandika Kihonda Oil Com kwa bao 1-0 kwa shida likikwamishwa wavuni na mshambuliaji wao tegemeo, Hamis Makame wakati mchezo baina ya timu ya Veteran ya Ukonga katika Jiji la Dar es Salaam na Bigwa ambapo katika mchezo huo Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa bao 1-0. Alisema Nahd.

Kwa uapnde wa michezo ya baiskeli Nahd alisema kuwa mwendesha baiskeli mkazi wa Chamiwno, Witiness Amani aliweza kuibuka mshindani wa kwanza baada ya kuwashinda wenzake 11 katika mbio za kilometa 40 zilizoanzia msikiti wa Karume, Mzumbe na kumalizikia katika chuo kikuu cha Waislam.

Katika mbio za waendesha upande wa walemavu, Juma Habibu aliibuka mshindi kwa kushika nafasi ya kwanza akiwashinda wenzake tisa katika mbio kilometa sita zilizoanzia katika msikiti huo wa Karume na kumalizika katika chuo hicho.

“Tamasha hili limekuwa na mafanikio makubwa sana hasa baada ya kupata washiriki kutoka Dar es Salaam, Pwani na wenyeji Morogoro na tumefanikiwa kuwashirikisha waumini wa dini ya kiislam na kushiriki michezo aina mbalimbali wakiwemo na walemavu ambao nao walikuwa na mashindano yao hii ni faraja sana upande wetu”. alisema Mwenyekiti huyo.

Nahd alisema kuwa licha ya kuwepo kwa michezo hiyo kulikuwa na michezo mingine ikiwemo michezo ya salakasi kutumia baiskeli, vikundi vya kareti kutoka ndani ya Manispaa ya Morogoro na michezo ya akinamama na watoto ambao nao walitapata fursa ya kubembeaambapo michezo hiyo ilifanyika kuanzia majira ya saa 7 mchana hadi saa 12 jioni.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: