Wanajeshi wa Kenya wakijiandaa kupanda lori kuelekea Liboi, Kenya karibu na mpaka na Somalia.
ZAIDI ya raia 50 kutoka jamii ya Pokomo katika kijiji
kimoja katika eneo la Reketa nchini Kenya wanadaiwa kufariki dunia baada ya
watu wenye silaha waliposhambulia wanakijiji hicho.
Kufuatana na mwenyekiti wa baraza la utawala la wilaya ya Mto Tana Diwani Salim Ngolo alisema kuwa leo ni siku ya huzini mkubwa kabisa kwa sababu watu wasio na hatia waliweza kumalizwa na kundi haramu.
Ngolo alisema kuwa katika kijiji chake kina watu 68 wameuwawa.
Diwani huyo alisema kuwa kundi la watu walivamia nyumba za watu wakati wa usiku na kutia moto na kuwashambulia kwa mapanga wale walojaribu kujinusuru na tukio hilo la moto.
Diwani huyo alisema kuwa kundi la watu walivamia nyumba za watu wakati wa usiku na kutia moto na kuwashambulia kwa mapanga wale walojaribu kujinusuru na tukio hilo la moto.
Jeshi la polisi wa mkoa wa Pwani katika taarifa ya kwa vyombo vya habari vielezea kuwa idadi ya walofariki dunia ni watu 48 wengi wao wakiwemo wanawake na watoto.
0 comments:
Post a Comment