BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MEYA MANISPAA YA MOROGORO AZINDUA MASHINDANO YA KAMANDA SHILOGILE CUP 2012 UWANJA WA SHUJAA.

MEYA MANISPAA YA MOROGORO AKIFUNGA PENALTI WAKATI WA UZINDUZI WA MASHINDANO YA SHILOGILE CUP 2012 UWANJA WA SHUJAA.
 
MEYA wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo akipiga mpira katika lango kufunga penalti wakati ikiwa ni ishara ya kuzindua mashindano ya Kamanda Shilogile CUP 2012 katika michezo iliyobeba ujumbe wa ulinzi shiriki polisi jamii katika uwanja wa Shujaa Manispaa mkoani hapa.
Kiungo mshambuliaji wa timu ya soka ya Boma SC, Winston Sanga (jezi ya kijani) akiwatoka wachezaji wa timu ya soka ya kata ya Mafiga FC Ezra Julius kushoto na Hassan Hamis wakati wa ufunguzi wa mashindano ya ulinzi shiriki polisi jamii (Kamanda Shilogile Cup 2012) katika uwanja wa Shujaa Manispaa ya Morogoro ambapo katika mchezo huo Boma SC ilishinda kwa bao 3-0.
 Mshambuliaji hiyo ya timu ya soka ya kata ya Boma SC, Athman Kidumke (mbele) akimiliki mpira dhidi ya mlinzi wa timu ya kata ya Mafiga FC, Yunusi Dadi ambapo mshambuliaji huyu alifunga mabao mawili pekee yake katika mchezo huo.

MICHEZO ya mashindano ya kombe la ulinzi shiriki polisi jamii yameanza kutimua vumbi baada ya timu ya soka ya kata ya Mafiga FC kukubali kipigo kutoka kwa vijana wa timu ya kata ya Boma SC katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo maarufu Kamanda Shilogile Cup 2012 kwa kutandikwa bao 3-0 mchezo uliofanyika uwanja wa Shujaa Manispaa ya Morogoro.

Katika mchezo huo dalili za ushindi kwa timu ya soka ya kata ya Boma SC zilianza kuonekana mapema hasa baada ya kutawala sehemu kubwa ya kiungo huku ikitandaza soka safi na kuvutia na lenye kasi huku wakitengeneza nafasi nyingi za mabao kutokana na wapinzani hao kupwaya eneo hilo hali iliyosababisha kushindwa kuendena na kasi ya mchezo huo.

Timu ya Boma SC walipata mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa mshambuliaji wao tegemeo, Athuman Kidumke aliyefanikiwa kukwamisha nyavuni bao mbili pekee yake akifunga dakika ya 41 baada ya kushirikiana vema na Waziri Bakari wakati bao la pili akifunga dakika ya 48 kufuatia pasi ya kiungo mshambuliaji Winston Sanga na kufunga mabao hayo.

Bao la tatu lilifungwa kwa njia ya mkwaju wa penalti na mshambuliaji, Abdallah Matokeo kufuatia kuangushwa kwa mshambuliaji, Salum Mzangi na mlinzi wa timu ya Mafiga FC na mwamuzi wa mchezo huo, Mohamed Teophil kutoa adhabu hiyo na kuandika bao la tatu na ushindi kwa timu yake katika mchezo huo.

Naye Mratibu wa mashindano hayo, Mussa Ng’amba alisema kuwa katika mashindano ya mwaka huu yameboreshwa kwa kiasi kikubwa hasa kwa kubadilisha mfumo uliozoeleka ambao ulikuwa ukishirikisha timu kutoka ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa.

"msimu wa mwaka jana katika mashindano hayo tulishirikisha timu zinazoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa lakini mwaka huu tumebadilisha kwa kuchukua timu zilizopo ndani ya kata husika na kuwa mwaka jana pia kuliwa na timu za vijana chini ya umri wa miaka 17 na umri chini ya 23 ambao kwa sasa wamekuwa wamechanganywa katika timu hizo za kata ili nao wapate uzoefu". alisema Ng'amba.

Alisema kuwa mashindano hayo yameshirikisha timu kutoka katika kata 24 na timu za vijana chini ya umri wa miaka 14 na kuwa lengo hilo ni kutaka kuwaibua na kuwaendeleza katika taasisi mbalimbali za ndani na nje ya mkoa wa Morogoro.

Ng’amba alisema kuwa mashindano hayo yamegawanywa katika makundi manne na ambapo hatua ya makundi mzunguko wake unatarajia kumalizika septemba 20 na fainali zake kufanyika septemba 29 mwaka huu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: