BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANDISHI WA HABARI WA SOMALI AUAWA.

Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia. 
WATU wenye silaha wamemuuwa mwandishi wa habari maarufu wa Somalia eneo ambalo limekuwa hatari kwa watu wenye taaluma hiyo duniani.

Katika tukio hili watu wasiojulikana jana walimuuwa kwa kumfyatulia risasi, Yusuf  Ali Osman anayejulikana  sana kwa jina la farey katika wilaya ya dharkenely mjini Mogadishu .


Osman mkurugenzi wa zamani  wa radio Mogadishu alikuwa anafanya kazi katika wizara ya habari ya Somalia.


Jumuiya ya waandishi wa habari wa somalia iliyoko uhamishoni nchini Kenya katika taarifa yake ili sema kuwa Osman ni mwandishi wa habari wa nane kuuwawa nchini somalia katika kipindi cha mwaka 2012. 

katika taarifa hiyo jumuiya hiyo ilisema kuwa inaumiza na kuvunja moyo hasa kwa kuwapoteza mwandishi wa habari mahiri kila mwezi.

Mwakilishi maalumu wa umoja wa mataifa  kwa ajili ya Somalia Augustine Mahiga alilaani kuuwawa  kwa Osman na kutoa mwito tena kwa maafisa wa Somalia kufanya uchunguzi wa mashambulizi kwa waandishi wa habari.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: