BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SAKALA LA MELI ZA IRAN KUTUMIA BENDERA ZA TANZANIA, TANZANIA YADAIWA INAKUSUDIO LA KUFUTA SAJILI YA MELI ZA NCHI YA IRAN.

BENDERA YA TANZANIA
 SERIKALI ya Tanzania inasema kuwa meli za mafuta 36 za Iran zimesajiliwa tena nchini Tanzania ili kujaribu kuhepa vikwazo dhidi ya Iran vilivowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya.

Katika uchunguzi uliofaywa na serikali ya Tanzania ambao ulionekana na shirika la habari la Reuters unaonesha kuwa serikali haikujua lolote kuhusu shughuli hizo za kuzipatia meli za mafuta za Iran bendera ya Tanzania na kuwa shughuli iliyokuwa ikifanywa na wakala alioko Dubai.

Mafuta ya Iran yamewekewa vikwazo ili kuishawishi Iran iache mradi wake wa nuklia.

nchi ya Tanzania inadaiwa imeacha kuagiza mafuta kutoka nchi ya Iran.

Uchunguzi huo ulifanywa na serikali ya Tanzania baada ya mbunge mmoja wa Marekani, Howard Berman, mwenyekiti wa kamati ya Congress ya maswala ya nchi za nje kueleza kuwa wasiwasi wake juu ya meli hizo za Iran kupatiwa bendera ya Tanzania.

Tanzania sasa inasema kuwa itafuta usajili wa meli hizo.

habari hii kwa mujibu wa idhaa ya sauti ya afrika kutoka nchini-Cairo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: