Polisi katika mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana unaoendeshwa na kampuni ya Lonmin , ambayo ni kampuni ya tatu duniani kuzalisha madini hayo, badala yake walichukua tahadhari ya kujilinda dhidi ya mamia ya wafanyakazi ambao walivamia huku wakishambuliwa kwa mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira wakijaribu kuwashambulia maafisa wa polisi kwa bunduki, mapanga na marungu.
Lakini taifa hilo lilijikunyata katika kile ambacho vyombo vya habari vimelieleza haraka tukio hilo kuwa ni "Mauaji ya Marikana", wakilinganisha tukio hilo na mauaji ya wakati wa enzi za utawala wa kibaguzi, hususan mauaji ya Sharpeville ya mwaka 1960 wakati polisi wa utawala huo wa wazungu walipowauwa waandamanaji 69.
Zuma asitisha ziara
Wakati idadi ya waliouwawa ikiongezeka jana , Zuma alifupisha ziara yake katika mkutano wa kimkoa na kurejea nyumbani na moja kwa moja alikwenda katika mgodi huo, akiaahidi kufichua sababu za mauaji hayo.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma
Ni wazi kuwa kuna kitu nyuma ya matukio haya na ndio sababu nimechukua uamuzi huu wa kuunda tume ya uchunguzi, kwa sababu ni lazima tujue ukweli, Zuma amesema.
Hiki ni kitu kinachositua, Hatufahamu kinatokea wapi na ni lazima tufahamu. Hali hii haikubaliki nchini mwetu, ambayo ni nchi ambayo kila mtu anajisikia salama.
Nchi ambayo ina demokrasia ambayo kila mtu anaionea kijicho.
Polisi wa Afrika kusini wakipita karibu na maiti baada ya kuwafyatulia risasi karibu na mgodi Marikan.
MAREKANI YASIKITIKA
Ikulu ya Marekani , White House, imesema jana Ijumaa kuwa Marekani imesikitishwa na vifo na kueleza matumaini kuhusu uchunguzi wa serikali. Watu wa Marekani wamesikitishewa na vifo vilivyotokea , amesema naibu afisa wa habari wa ikulu ya Marekani Josh Earnest alipokuwa akizungumza na waandishi habari.
Tunaimani kuwa serikali ya Afrika kusini itachunguza mambo yaliyosababisha hali hii na kila wakati, tunazipa moyo pande zote kufanyakazi kwa pamoja kuipatia ufumbuzi hali hii kwa amani.
Mwanamke alia baada ya polisi kuuwa wachimba migodi katika mgodi wa Lonmin Platinum Afrika Kusini, Agosti 17, 2012.
MKUU WA POLISI ASEMA:
Mkuu wa polisi Riah Phiyega amewakingia kifua maafisa wake wa polisi , akisema kuwa walitumia risasi baada ya majadiliano na mbinu za kulidhibiti kundi hilo la wachimba migodi kushindwa.
Kundi hilo la wanaharakati lilikimbia kuelekea kwa polisi, wakifyatua risasi na kuwa na silaha hatari, amesema.
Polisi walirudi nyuma kimpango na walilazimika kutumia nguvu kiasi kujilinda. Hadi sasa watu 259 wamekamatwa kuhusiana na mapambano hayo ambayo yamesababisha watu 34 kuuwawa na wengine 78 wamejeruhiwa, amesema Phiyega.
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo walikuwa katika mgomo wa wiki moja wakidai nyongeza mara tatu ya mishahara yao kutoka randi 4,000 ambayo ni sawa na euro 400 kwa mwezi.
0 comments:
Post a Comment