Mwenyekiti huyo wa Morogoro Musilim Kumbat Jamaat Alhaj, Bachoo Sadik Bachoo akimkabidhi Hamza Omari.
Nuru Makusi kushoto akikabidhiwa msaada huo na mgeni rasmi Bachoo Sadik Bachoo katika hafla hiyo.
TAASISI ya kiislam ya Jabal-Hira seminary ya Mkoani Morogoro imetoa msaada wa vyakula vya aina mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 2.6 milioni kwa makundi ya walemavu na yatima kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya Idd Elfitri.
Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo kwa waumini wa dini ya kiislam ambao ni walemavu na yatima Mwenyekiti wa Taasisi ya Morogoro Muslim Kumbar Jamaat, Alhaj Bachoo Sadik Bachoo (Malaika) alisema msaada huo umetolewa kwa kuzingatia mahitaji ya makundi mbalimbali ya watu wasiojiweza ili nao waweze kusherehekea sikukuu ya Idd-Fitri baada ya waumini wa dini hiyo kutoa sadaka katika mfungo wa ramadhani.
Bachoo alisema mfunmo huo wa kutoa misaada kwa makundi kama hayo ya yatima na walemavu yamelenga kuwawezesha kila mumuumini wa dini hiyo hasa katika sikukuu ya idd fitri na siku nyingine kusherehekea vizuri baada ya kupokea misaada hiyo kutokana na matatizo walionayo.
“Sadaka hii imetolewa kwa wakati muafaka kwani lengo kuu ni kuwa nanyi muweze kusherehekea sikukuu ya idd-fitri hasa kwa kupiga chakula kizuri baada ya waumini wenzenu kutoa sadaka katika mwezi huu wa ramadhamani nafikiri itasaidia sana kuwapungua baadhi ya kero siku ya idd-fitri” alisema Bachoo.
Naye Katibu wa taasisi hiyo ya kiislam ya Jabal-Hira seminari Morogoro, Hemedi Mkuya alisema kuwa taasisi hiyo imekusanya zaidi ya nusu tani ya vyakula mbalimbali vikiwemo sukari, mchele, maharage, ngano unga na mafuta ya ya kupikia vyote zikiwa na thamani ya sh2.6Mil.
Mkuya alisema kuwa mgao huo kwa makundi hayo utawafikia walenga takribani waumini 90 ambao kila mmoja wao atapokea jumla ya kilo 11 za vyakula mbalimbali na kuwa wastani wa kaya mmoja yenye watu zaidi ya watano ama saba katika familia sadaka hiyo watafaidika zaidi ya watu 340.
0 comments:
Post a Comment