YAAQUB NAHD NIPO KATIKA SALA: Mtoto Yaaqub Nahdi Aref (2) akiwa katika sala ya Idd el Fitri na waumini wa dini ya kiislam inayosaliwa kufuatia kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani ambapo waumini wa dini ya kiislam wanaungana na waislam wenzao duniani kote kusherehea sherehe za sikukuu hiyo hapa nchini iliyofanyika kwenye viwanja vya The Islamic Foundation kata ya Boma mkabara na hoteli ya Hilux Manispaa ya Morogoro.
SALA YA IDD EL FITRI: Waumini wa dini ya kiislam wakiwa katika sala ya Idd El Fitri katika viwanja vya The Islamic Foundatin. |
TENDENI MEMA: Shekhe Juma Mohamed Amiri akiwahutubia waumini wa dini ya kiislam mara baada ya kumalizika kwa sala ya Idd El Fitri katika viwanja hivyo. |
FURAHA: Viongozi wa juu wa taasisi ya Islamic Foundation wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Aref Nahd kulia aliye na mtoto Yaaqub Nahdi Aref (2) wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa sala ya Idd El Fitri, kushoto mbele ni Meneja wa redio Iman, Mohamed Matano.
UFAFANUZI: Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic
Foundation Morogoro Nahdi Aref
akiwa na mtoto wake Yaaqub Nahdi Aref (2) akijieleza jambo kwa Jafari Mponda kulia wakati Mwenyekiti huyu akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa sala ya Idd el Fitri
SHEKHE TUNAKUSIKILIZA: Waumini wakifuatalia hutuba ya idd el fitri ilikuwa ikitolewa na Shekhe Juma Mohamed Amiri katika viwanja hivyo vya Hilux
TUNAFUATILIA HUTUBA: Waumini wa dini ya kiislam wanawake nao wakiwa katika sehemu maalum huku wakifuatilia hutuba hiyo.
0 comments:
Post a Comment