BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAUMINI WA DINI YA KIISLAM MOROGORO, PWANI NA DAR ES SALAAM WALIVYOADHIMISHA SHEREHE ZA IDD EL FITRI.

 Mwendesha baiske ya magurudumu mawili akionyesha uhodari wa kumruka mtu (aliyelala chini) wakati wa tamasha la michezo la Idd El Fitri lililofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha kiislama Manispaa ya Morogoro na kuhudhuliwa na waumini wa mikoa ya Dar es Salaam, na Pwani.
 Mussa Ramadhan (12) mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Daru Argam akionyesha uhodari wa kuendesha baiskeli ya gurudumu moja wakati wa tamasha la Idd El Fitri.
 Mshindi namba mbili wa mbio za baiskeli za magurugudumu matatu, Seleman Matandiko akionyesha mbwembwe wakati akimaliza mbio hizo.
 mshindi namba moja katika mbio za kilolmeta 40, Witiness Aman akimaliza mbio hizo
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislam ya The Islamic Foundation Tanzania, Aref Nhd kulia akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa BagamoyoIdd Kiboksi ambpo katika mchezo timu ya Mwenyekiti huyo ilikubali kichapo cha bao moja lililofungwa na mchezaji huyo wa Bagamoyo.
 Timu ya kuvuta kamba ya wachezaji mchanganyiko kutoka Jiji la Dar es Salaam wakionyesha uwezo mkubwa dhidi ya wapinzani wao (hawako pichani) wa Morogoro ambapo Morogoro walishindwa kwa kuvutwa mara moja na kuwaachia ushindi wenzao wa Dar es Salaam.
 NYIE MWAACHE KUKU WANGU HUYU: Mtoto Seleman Ayoub (12) akijaribu kuwadhibiti wenzake ili wasimpokonye kuku wake aliyedai kumkamata wakati wa shindano la kufukuza na kukamata kuku katika tamasha hilo.

 Sehemu ya waumini wa dini ya kiislama wakifuatilia matukio mbalimbali yalikuwa yakiendelea kwenye viwanja hivyo.
 Sehemu ya wanawake na watoto wakifuatilia matukio mbalimbali yalikuwa yakiendelea kwenye viwanja hivyo.
 Msimamizi wa Michanga Redio na TV Imani, Ahmed Omari Bawazir kulia akimsikiliza mmoja wa wageni waliohudhuria tamasha hilo katika meza kuu.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislam ya The Islamic Foundation Tanzania, Aref Nhd (mwenye fulana ya blue) akihesabu pesa kwa ajili ya kumkabidhi mshindi wa kwanza mbio za baiskeli Witiness Aman wakati wa zoezi la utoaji wa zawadi kwa washindi wa tamasha hilo, wa pili kutoka kushoto ni Msimamizi wa Michanga Redio na TV Imani, Ahmed Omari Bawazir. na kulia ni Meneja wa kituo cha redio Iman, Mohamed Matano.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: