Wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Bungo Manispaa ya
Morogoro wakifanya usafi kwa kufuta katika madawati katika moja ya darasa ya shule
hiyo kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mitihani ya taifa ya kuhitimu elimu ya
msingi inayoanza kesho nchini kote.
Sehemu ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Bungo Manispaa ya Morogoro wakiweka namba katika madawati ikiwa maandalizi ya mitihani ya taifa ya kuhitimu elimu.


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bungo Manispaa ya Morogoro, Roman Luwoga akihakiki fomu za maombi ya wanafunzi wa darasa la saba (TS9) kwa ajili ya maandalizi ya kujiunga na masomo ya elimu ya sekondari mara baada ya kuhitimu elimu ya darasa la saba ambapo kesho wanafunzi wa darasa la saba wanafanya mitihani ya kuhitimu elimu hiyo nchini kote.
0 comments:
Post a Comment