Wazazi wanaruhusia tu kupata mtoto mmoja nchini China.
AFISA mmoja mkuu nchini China ameachishwa kazi
kufuatia madai kuwa alivunja sheria ya ya ndoa ya nchi pamoja na sheria
ya kuruhusiwa tu kuwa na mtoto mmoja.
Inaarifiwa kuwa afisaa huyo, Li Junwen alivunja sheria kwa kuwa na wake wanne na watoto kumi.
Vyombo
vya habari vya serikali vinasema kuwa bwana, Li Junwen, alipata watoto
wanne na mke wake wa kwanza na tayari alikuwa ameishi na wanawake
wengine watatu ambao alipata nao watoto waliosalia.
Maafisa wanasema anachunguzwa kwa kosa hilo ingawa kusheria haileweki uhusiano aliokuwa nao na wanawake hao.
China inaruhusu tu wazazi kuwa na mtoto mmoja la sivyo walipe faini kwa serikali kila mtoto wa ziada.
Inajulikana kuwa wanawake wengi nchini China hulazimishwa kutoa kimba zao wanapojulikana kuwa na mbimba ya pili.
0 comments:
Post a Comment