WAMISRI leo Jumamosi Dec 15/ 2012 wanapiga kura ya maoni kuhusu rasimu
ya katiba yao mpya iliyoidhinishwa na wanasiasa wanaoyaunga mkono ya
makundi ya Kiislamu kama njia ya kujitoa kutoka katika mzozo wa kisias.
Makundi hayo ya vyama vya Kiislamu yanatupilia mbali tuhuma za wapinzani
kuwa rasmu hiyo ya katiba ni chachu ya mgawanyiko zaidi katika taifa
hilo kubwa la Kiarabu.
Upigaji kura umeanza leo katika mswada wa katiba ulioligawa taifa hilo,
ambapo mzozo huo umekuwa kati ya waungaji mkono wa makundi ya Kiislamu
yanayomuunga mkono rais Mohamed Mursi dhidi ya waliberali, wale
wanaotaka kutenganishwa kwa dini na serikali pamoja na Wakristo katika
mapambano ambayo mara kwa mara yamesababisha umwagikaji wa damu mjini
Cairo pamoja na miji mingine.
Maandamano ambayo yamekuwa na vurugu
Upinzani unasema kuwa katiba hiyo inaelemea zaidi katika matakwa ya
Kiislamu na inakanyaga haki za wachache.
Waungaji mkono wa Mursi
wanasema katiba hiyo inahitajika iwapo maendeleo yatafikiwa kuelekea
demokrasia karibu miaka miwili baada ya kuanguka kwa utawala wa kijeshi
wa Hosni Mubarak.
Mjini Alexandria jana Ijumaa(14.12.2012) hali ya wasi wasi ilitanda na
kusambaa hadi kuwa mapambano ya mitaani baina ya makundi hasimu ambayo
yamekuwa na marungu, visu, na panga.
Waungaji mkono wa Mursi walijitokeza pia mjini Cairo.
Magari yachomwa moto
Magari kadha yamechomwa moto na mhubiri mmoja wa dini ya Kiislamu ambaye
alitoa wito kwa watu kupiga kura ya ndio kwa katiba hiyo alikwama ndani
ya msikiti baada ya kuzingirwa na wafuasi wa upinzani ambao walikuwa na
hasira.
Katika mji mkuu , Cairo, pande zote mbili zilifanya juhudi za wastani za mwisho kuwashawishi waungaji wao mkono.
Mapambano mjini Alexandria baina ya waandamanaj.
Makundi ya waungaji mkono vyama vya Kiislamu yakipunga bendera ,
yalijikusanya kwa amani katika msikiti mmoja mkubwa , baadhi wakiimba ,
"Uislamu, Uislamu" na "Tumekuja hapa kusema "NDIO", kwa katiba".
Waungaji mkono wa upinzani , ambao wametakiwa kupiga kura ya "HAPANA",
na viongozi wao, walijikusanya nje ya ikulu ya Misri mjini Cairo.
Jengo hilo linaendelea kuzingirwa na polisi, wanajeshi na vifaru vya
jeshi baada ya mapambano ya mitaani kusababisha kiasi ya watu wanane
kuuwawa mapema mwezi huu katika ghasia zilizosababishwa na uamuzi wa
rais Mursi kujipa madaraka makubwa ili kuweza kupitishwa kwa rasmu ya
katiba mpya.
Wakati giza linaanza kutanda , kulionekana tu watu ambao walikuwa
wakiangalia hali ya mambo pamoja na wachuuzi katika eneo hilo badala ya
waandamanaji.
Waandamanaji mjini Cairo.
Mursi ashambuliwa
Mwanamke mmoja alikuwa akiliambia kundi la watu kupitia kipaza sauti,
akitoa matusi kwa Mursi, lakini wengi wa watu waliokuwa wakimsikiliza
hawakuonekana kujali anayosema na kuendelea kunywa chai ama kupiga picha
mbele ya kifaru.
"Simpendi Mursi," amesema Moustafa Ahmed , mwenye umri wa miaka 25, na
mwalimu.
"Lakini sijaamua jinsi nitakavyopiga kura , kwa hiyo nimeamua
kuja hapa kusikiliza waandamanaji na kuzungumza nao kwa mara ya mwisho."
0 comments:
Post a Comment