BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BABA MTAKATIFU AIOMBEA AMAN MASHARIKI YA KATI KATIKA MISA YA MKESHA WA KRISMASI VATICAN.

Baba Mtakatifu Benedict akisalia misa ya mkesha wa Kristmas katika kanisa la St. Peter's Basilica Vatican Dec. 24, 2012
Baba Mtakatifu Benedict akisalia misa ya mkesha wa Kristmasi katika kanisa la St. Peter's Basilica Vatican jana.


BABA Mtakatifu Benedict ameombea amani, hasa Mashariki ya Kati, katika misa yake ya mkesha wa Krismas, wakati wakristo kote duniani wanajiandaa kusherehekea leo kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.

Akihutubia waumini katika kanisa la Mtakatifu Petro Jumatatu jioni, kiongozi huyo wa kanisa katoliki alitoa wito wa kumaliza umwagaji damu Syria, Lebanon, Iraq na nchi za jirani. 


Aliombea pia watu wa Israel na Palestina kuishi pamoja kwa amani.

Maelfu wa watalii kutoka kote duniani walikusanyika katika mji wa Bethlehem, Ng'ambo ya Magharibi kusherehekea sikukuu hiyo mahali ambapo Wakristo wanaamini Yesu Kristo alizaliwa.


Jumanne maelfu ya Wakristo kote duniani watamiminika katika makanisa kuhudhuria misa ya krismas na kufuatiwa na sherehe ikiwa ni chakula, vinywaji na kutembeleana. 
Katika nchi za Afrika Mashariki na Kati wakristo wengi wanatazamiwa kusherehekea kwa mikusanyiko ya kila namna kuanzia starehe hadi ibada.

Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika inawatakiwa wasikilizaji wetu wote Krismas Njema
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: