BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NELSON MANDELA KULA KRISMASI HOPSITALINI.

RAIS MSTAAFU WA AFRIKA YA KUSINI NELSON MANDELA.
Mzee Nelson Mandela kushoto akisalimiana na Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton miaka ya hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini.


SERIKALI ya Afrika Kusini imetangaza kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Nelson Mandela atasalia hospitalini msimu huu wa Krismasi.

Mzee Mandela ambaye ni rais mweusi wa kwanza nchini Afrika Kusini, alilazwa hospitali wiki mbili zilizopita kufuatia maambukizi ya mapafu na uvimbe au mawe kwenye kibofu.
Kuna wasi wasi mkubwa nchini Afrika kuhusu afya yab rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 94.

Mandela alifungwa miaka 27 baada ya kupatikana na hatia ya kuongoza uasi dhidi ya serikali ya Wazungu walio wachache nchini humo.

Raia wengi wa nchi hiyo wanamuona kama baba wa taifa kutokana na juhudi zake ya kupigania uhuru wa taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali, Bwana Mandela atasherehekea siku kuu ya Krismasi akiwa hospitalini.
Mwandishi wa BBC, mjini Johannesburg, anasema kila kukicha kuna hali ya wasi wasi kuhusu afya ya rais huyo wa zamani.

Awali kulikuwa na matumaini kuwa Bwana Mandela huenda akaruhusiwa kwenda nyumbani, lakini madaktari wake wanasema hawako tayari kumruhusu Bwana Mandela kwenda nyumbani.

Licha ya rais Zuma kutangaza kuwa Afya ya rais huyo wa zamani sio nzuri sana, Rais Zuma amesema anaendelea kupata nafuu.
Serikali ya Afrika Kusini imesema Mandela anatibiwa kufuatia maambukizi ya Mapafu katika hospitali moja mjini Pretoria.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: