KWA UFUPI
Alisema wanaCCM wanapaswa kutembea kifua mbele kwa sababu chama chao kimefanya vizuri sana katika kutekeleza ahadi zake na nyingine zilizobaki zitaendelea kutekelezwa, Akitolea mfano Jimbo la Segerea na Kata ya Tabata, ambako alisema barabara kadhaa zimekarabatiwa na nyingine ziko kwenye mikakati ya kujengwa kwa lami na changarawe.
MBUNGE wa Segerea, jijini Dar es Salaam, Dk Makongoro Mahanga amesema rushwa na ufisadi ndiyo ajenda pekee ya vyama vya upinzani katika kukichafua CCM na kuitumia kama hoja ya kutaka kukiondoa madarakani katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Dk Mahanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, alisema baada ya viongozi wa CCM na Serikali kuanza kwa nguvu kuusemea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, wananchi wengi wametambua kwamba chama hicho na Serikali yake imetekeleza miradi mingi ya maendeleo kote nchini.
Aliyasema hayo juzi alipokuwa akifunga semina ya viongozi wa mashina ya CCM katika Tawi la Mtambani, Kata ya Tabata.
Alisema wanaCCM wanapaswa kutembea kifua mbele kwa sababu chama chao kimefanya vizuri sana katika kutekeleza ahadi zake na nyingine zilizobaki zitaendelea kutekelezwa.
Akitolea mfano Jimbo la Segerea na Kata ya Tabata, ambako alisema barabara kadhaa zimekarabatiwa na nyingine ziko kwenye mikakati ya kujengwa kwa lami na changarawe.
Mbunge huyo alizitaja barabara hizo kuwa ni pamoja na ya Vingunguti Darajani hadi Baracuda, Barabara ya St Marys na Barabara ya Kisiwani ambayo daraja limejengwa.
Pia alisema visima na mtandao wa maji vimewekwa katika Kata ya Tabata, licha ya ujenzi wa shule za msingi na Shule ya Sekondari ya Zawadi inayoendelea kuongezewa madarasa.
Dk Mahanga alisema kwa sasa hata wapinzani wametambua kwamba kauli ya “CCM haijafanya lolote” haiwezi kuwasaidia kwa sababu ni ya uwongo.
Hata hivyo alikiri kuwa rushwa na ufisadi ni tatizo ndani ya vyama na ndani ya Serikali.
Alizitaja kata mbili za Kimanga na Segerea katika Jimbo la Segerea ambazo ndiyo kata mbili pekee kati ya kata 26 za Wilaya ya Ilala zilizochukuliwa na wapinzani mwaka 2010 zitarejeshwa CCM mwaka 2015.
Dr Mahanga alisema kero mbili kuu za maji na barabara katika Jimbo la Segerea zitashughulikiwa na kutatuliwa ndani ya miaka mitatu ijayo kama alivyoahidi kwenye kampeni zake za mwaka 2010.
Aliwashukia baadhi ya wapinzani wanaobeza utendaji wake akisema anatekeleza ahadi zake kisayansi na kwa umakini wa hali ya juu na ikifika mwaka 2015, atawakata kilimilimi wapinzani wake hao. Aliahidi kwamba siku chache zijazo ataweka wazi mambo yote yaliyotekelezwa katika Jimbo la Segerea katika kipindi cha miaka miwili toka Novemba 2010 hadi Oktoba 2012.

0 comments:
Post a Comment