Wanamgambo wa Free Syrian Army wakimkashifu Rais Al-
Assad.
KUNA uwezekano kwamba serikali ya Syria inaweza kushindwa na majeshi ya upinzani wakati wowote ule, naibu waziri wa masuala ya kigeni wa Urusi amesema.
Wanajeshi wa rais Bashar al-Assad "wanazidi kupoteza maeneo zaidi kila wa leo", Mikhail Bogdanov alisema Alhamisi, kulingana na mashirika ya habari ya Urusi.
Urusi imekuwa mmojawapo wa washirika wakuu wa serikali ya Bwana Assad.
Wakati huohuo, Urusi inafanya mipango ya kujitayarisha kuwahamisha maelfu ya Warusi toka Syria, Bwana Bogdanov alisema.
Mlipuko
"Kwa kweli hatuwezi kutupilia mbali uwezekano wa kwamba waasi wa Syria wanaweza kushinda," Bwana Bogdanov alisema.
Nchini Syria kwenyewe, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kutokea kwa mlipuko katika eneo la Qatana, jijini Damascus, ambalo limewaua watu 16, wakiwemo watoto saba.
0 comments:
Post a Comment