BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

GEORGE H.W.BUSH ALAZWA KATIKA CHUMBA CHA GONJWA MAHUTUTI-ICU, CHANZO NI TATIZO LA UPUMUAJI.


RAIS wa zamani wa Marekani, George H.W.Bush amelezwa kwenye  chumba  cha wagonjwa mahtuti -ICU katika hospitali moja huko Houston katika jimbo la Texas nchini Marekani.

Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 88 alilazwa hospitalini mwezi uliopita  akiwa na tatizo la kupumua.George H.W. Bush akiwa na mkewe Barbara na wajukuu zao, Barbara(Kushoto) na Jenna
George H.W. Bush akiwa na mkewe Barbara na wajukuu zao, Barbara(Kushoto) na Jenna.

Msemaji wake anasema bwana Bush alihamishiwa kwenye  chumba cha wagonjwa mahututi Jumapili  baada ya kupata homa kali. Aidha msemaji huyo anasema rais huyo wa zamani anaendelea kuangaliwa kwa karibu na kwamba madaktari wana matumaini kuhusu matibabu yake.
Mkewe Barbara Bush na mtoto wake mmoja wa kiume pamoja na mjukuu wa kiume walisheherekea sikukuu ya  Krismas hospitalini hapo na bwana Bush.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: