BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASTAR 27 WA YANGA SPORT CLUB KUJINOA UTURUKI IKIWA NI MAANDALIZI YA MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU VODACOM KUKWEA PIPA KESHO.


NYOTA 27 YANGA SC KUKWEA PIPA LA UTURUKI USIKU WA JUMAMOSI


KIKOSI cha wachezaji 27 wa Yanga Sc kinatarajiwa kuondoka nchini usiku wa jumamosi kuelekea nchini uturuki kwa ajili ya kuweka kambi maalum ya kujiandaa na mashindano mbalimbali.

Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Binkleb amesema  maandalizi ya safari hiyo yamekamilika na kwamba wachezaji watakaokwenda huko pamoja na viongozi watajulikana kesho.

Amesema kwamba kambi hiyo itakisaidia sana kikosi katika maandalizi yake ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom pamoja na michuano ya Kagame itakayofanyika Kigali, Rwanda ambapo Yanga ni bingwa tetezi.

"Ndo maana tumetaka kwenda Uturuki kwani huko kuna facilities nzuri kwa ajili ya kambi...pia huko tunataraji kiucheza mechi kadhaa za kirafiki,"amesema.

Yanga inayonolewa na Ernie Brandts jana ilichapwa bao 1-0 na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker Fc katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: