BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JK AWAKABA KOO WASOMI NA WATAALAMU, AWATAKA WAACHE KUBEZA SEKTA YA KILIMO.


RAIS DKT KIKWETE.



RAIS Jakaya Kikwete amezidi kuwakaba koo wasomi na wataalamu mbalimbali nchini kwa kuwataka kuacha kubeza sekta ya kilimo, badala yake wafanye utafiti kuinua sekta hiyo ili iwiane na sekta nyingine zinazokua kwa kasi.

Rais Kikwete, alitoa agizo hilo jana, wakati akifungua mkutano wa kujadili masuala ya uchumi, ulioandaliwa na Kigoda cha Wanataaluma cha Mwalimu Nyerere kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kitengo cha Uchumi.

Alisema sekta ya kilimo, imeendelea kudumaa kwa kuwa asilimia 75 ya mbegu za kilimo zinatoka nje ya nchi.


“Kwa kuwa mbegu hizi, zimezalishwa kulingana na hali ya hewa na mazingira ya nchi hizo, zikiletwa Tanzania haziwiani na hali ya mazingira ya nchi yetu na hivyo kuleta hasara kwa wakulima wetu, lakini yote haya yanatokana na utafiti mdogo unaofanywa na watafiti wazalendo.

“Hali hii, imekuwa ikichangia maendeleo ya wakulima kuendelea kuwa duni kwa kuwa asilimia kubwa ya Watanzania, wanategemea kilimo kwa ajili ya kujitafutia kipato.

“Kwa mfano sekta hii, imekua na kufikia asilimia nne pekee wakati zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanategemea sekta ya kilimo kwa maendeleo yao…. Hapa tunaona wazi sekta hii ni muhimu,” alisema Rais Kikwete.

“Lakini badala yake, watafiti wameendelea kufanya tafiti katika sekta za mawasiliano, sayansi, teknolojia, utalii na miundombinu ambazo zimechangia sekta hizi kukua kwa kasi.

“Ikumbukwe tafiti zinazofanywa na mashirika ya nje, hazina manufaa kwa taifa, bali ni kwa ajili ya wahisani, hadi kufikia 2015 tuna uhakika Serikali itakuwa ikitenga bajeti ya kutosha kufanya utafiti.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema katika mkutano huo wanatarajia kutoka na mapendekezo ambayo watayawasilisha kwa Rais Kikwete, ili yaanze kufanyiwa kazi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Delphin Rwegasira, alisema umefika wakati Watanzania kubadilika.


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: