BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JK:WENYE HILA NA CHUKI WANABEZA MAENDELEO YETU.


KWA UFUPI
“Utaratibu uliopo ni kuzungumza kila baada ya miaka mitano, lakini mwaka huu ninazungumza na wananchi kutokana na kuwapo kwa viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc). Nataka wasikie mafanikio yetu ya miaka 51 ya Uhuru,” alisema Rais Kikwete.Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto) Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein (kushoto), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange,Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, Wakiwa makini wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukiimbwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru jana.Picha na Salhim Shao.  


Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Uhuri akiwa kwenye gari maalum la Kijeshi na Sambamba na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange walipokuwa wakioa salamu kwa wananchi na wageni mbali mbali waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara.Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho Miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara,leo katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama kikitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakipokea salamu za heshima kutoka kwa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi la Usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo,kutoka kulia ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Mh. Joseph Kabila,Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji,Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.katikati ni Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda.
Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Kikosi cha wanaanga cha Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikitoa salamu za heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ) kikitoa salamu za heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii na heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.Picha na Full Shangwe Blog.
RAIS Jakaya Kikwete amesema wenye hila na chuki pekee ndiyo wanaosema kuwa Tanzania hakuna maendeleo.
Alisema hayo jana alipolihutubia Taifa kwenye maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
“Utaratibu uliopo ni kuzungumza kila baada ya miaka mitano, lakini mwaka huu ninazungumza na wananchi kutokana na kuwapo kwa viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc). Nataka wasikie mafanikio yetu ya miaka 51 ya Uhuru,” alisema Rais Kikwete.
Viongozi walioshiriki maadhimisho hayo ni marais Armando Guebuza wa Msumbiji, Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na Hifikepunye Pohamba wa Namibia.
Nchi zilizotuma wawakilishi katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na umati wa watu ni Lesotho, Zambia, Angola, Swaziland, Shelisheli, Rwanda, Zimbabwe, Mauritius na Malawi.
Rais Kikwete alisema mwenye macho hawezi kusema lolote, lakini kwa mwenye hila hakosi maneno na kutoa dosari kwa maendeleo yaliyofikiwa.
“Watu waliobahatika kuiona Tanzania ya mwaka 1961 wakija sasa hivi, wataona mabadiliko makubwa. Kuna mabadiliko makubwa na hii inatokana na kuboresha nyanja mbalimbali za kiuchumi, ulinzi na usalama na miundombinu... kwa wenye hila hawakosi la kusema ila mwenye macho haambiwi tazama,” alisema.
Aliwashukuru viongozi walioshiriki mkutano SADC… “Tumepata bahati ya uwepo wa viongozi waandamizi wa SADC baada ya kukubali ombi langu la kuhudhuria sherehe hizi japo wengine wametoa udhuru na kutuma wawakilishi,” alisema.
Viongozi mashuhuri wakosekana
Baadhi ya viongozi wa kitaifa wakiwamo wastaafu, hawakuwamo katika sherehe hizo.
Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na mtangulizi wa Kikwete, Benjamin Mkapa ambaye yuko Lushoto mkoani Tanga.
Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Idd ambao hata hivyo, haikuelezwa sababu za kukosekana kwao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: