BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KABOYONGA AFARIKI DUNIA, DKT KIKWETE AMLILIA.


Siraju Kaboyonga.

MBUNGE wa zamani wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga (CCM), amefariki dunia usiku wa kuamkia jana mjini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu, Sinza Mori jana, kaka mkubwa wa marehemu Haji Kaboyonga, alisema chanzo cha kifo cha marehemu ni ugonjwa wa shinikizo la damu na moyo lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu.

Alisema juzi saa 3:30 usiku, marehemu alikuwa na afya njema na baada ya kukamilisha shughuli zake alimwita mke wake na watoto, ili wamnyanyue kwa ajili ya kwenda kulala.

Alisema baada ya kubebwa katika kiti chake na kupelekwa chumbani, alilazwa kitandani akiwa hana nguvu.

“Kama mnavyojua, marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu kwa muda mrefu tangu alipopata ajali, lakini wakati wote afya yake ilikuwa safi na nzuri huku akiendelea na shughuli zake.

“Baada ya marehemu kufikishwa kitandani, aliishiwa nguvu na hakutamka jambo lolote, ndipo tulipobaini kuwa huenda presha (shikinizo la damu), imempanda tukamkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matatibu zaidi.

“Hata hivyo, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, ilipotimu saa 4:30, alifariki dunia na sasa tupo hapa kwa maandalizi ya mazishi yake,” alisema Haji.

Alisema katika kipindi chake cha uhai, marehemu siraju, alibahatika kuoa wake wawili na kujaliwa kupata watoto 12 pamoja na wajukuu sita.

Kaka huyo wa marehemu alisema kwa mujibu wa taratibu za dini ya kiislamu, marehemu ataswaliwa nyumbani kwake Sinza Mori na atazikwa leo katika makaburi ya Kisutu.

“Marehemu alijaliwa kuoa wake wawili ambao ni Mwema Pumzi na Nuru Kisesa, ambao wote kwa pamoja wamejaliwa kupata watoto na wajukuu,” alisema.

Mtoto wa marehemu anena

Akizungumzia kifo cha baba yake, mtoto wa nne wa marehemu Issa Siraju, alisema wakati wote wa uhai wa baba yao alikuwa akiwaasa kuwa na upendo na umoja katika maisha yao.

“Kuna mambo mengi sana ambayo ambayo mzee alikuwa akituhimiza watoto wake, hasa katika kuimarisha umoja kati yetu katika kila jambo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: