BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI HUVISA AIFUNGIA HOTELI YA KIMATAIFA YA DOUBLE TREE JIJINI DAR ES SALAA.


KWA UFUPI
“Nawataka kurekebisha mara moja mfumo huo wa majina kulipa faini kwa Baraza la Hifadhi na Uhifadhi wa Mazingira (Nemc),”alisema Dk Huvisa.Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa 

WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa, ameifunga Hoteli ya Kimataifa ya Double Tree, ya jijini Dar es Salaam, kutokana na kitendo cha kutiririsha maji machafu baharini.
Dk Huvisa alifanya hivyo jana baada ya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu wake, Charles Kitwanga.
Waziri alitembelea hoteli hiyo ili kuona utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kitwanga mapema mwezi huu, alipofanya ziara katika viwanda na hoteli zilizoko pembezoni mwa bahari, ili kuona mfumo wa majitaka.
“Nawataka kurekebisha mara moja mfumo huo wa majina kulipa faini kwa Baraza la Hifadhi na Uhifadhi wa Mazingira (Nemc),”alisema Dk Huvisa.
Dk Huvisa alifika hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa agizo lililotolewa na naibu wake wiki mbili zilizopita, halijafanyiwa kazi.
Alisema hoteli hiyo itafungwa hadi hapo itakapotekeleza agizo hilo na kuhakikisha kuwa majitaka hayatiririki baharini kama ilivyo sasa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: