CHIRISTOPHER Katongo ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa BBC mwaka wa 2012.
Naodha huyo wa Zambia mwenye miaka 30 amemshinda
Demba Ba, Didier Drogba, Younes Belhanda na Yahya Toure na kuwa mshindi
wa kwanza kutoka Kusini mwa Afrika katika historia ya mashindano hayo.
Orodha
ya washindani hao ilitengazwa na wataalamu wa soka Afrika, ambao
wamezingatia umahiri wa mchezaji, uwezo wa kiufundi na ushirikiano na
wachezaji wengine.
Na idadi kubwa ya watu wamepiga kura kupitia
njia ya mtandao au ujumbe mfupi huku asilimia 40 kati yao wakimchagua
Katongo, ambaye anachezea timu ya China Henan Construction.
Katongo aandikisha rekodi mpya
Huku wachezaji wote walioorodheshwa katika
kinyang'anyiro hicho walikuwa na mwaka mzuri, wanne kati yao walikuwa
wameshinda medali mbali mbali, ni Katongo pekee ambaye mafanikio yake
yamezingatiwa na mashabiki wa mpira Afrika.
Katongo, ambaye ni mwanajeshi nchini mwake,
alikuwa kivutio pindi alipoiongoza Zambia, katika michuano ya kombe la
Mataifa Bingwa barani Afrika mnamo mwezi wa Februari mwaka huu.
Alifunga magoli matatu katika fainali
iliyoandaliwa nchini Equatorial Guinea na Gabon na baadaye kufunga bao
la ushindi kupitia mkwaju wa penalti na kuisadia Zambia kunyakuwa kombe
hilo.
Zambia iliishindi Ivory Coast kwa 8-7 katika
fainali hiyo baada ya timu hizo mbili kutoshana nguvu baada ya muda wa
kawaida na muda wa ziada mjini Libreville.
Katongo afufua matumaini ya Zambia kuelekea Brazil
Kilikuwa ni kipindi kilichojawa na hisia kwa
Zambia, ambayo miaka 19, iliyopita ilipata msiba mkubwa, pale ndege
iliyokuwa imebeba wachezaji wa timu ya taifa ilipoanguka mita 500 tu
mbali na Libreville, na kuuwa wachezaji wote 25 na rubani wake.
Miezi saba baada ya kuongoza Zambia kushinda
kombe hilo, Katongo vile vile amekuwa nyota wa timu yake ya taifa wakati
wa michuano ya kufuzu kwa fainali za mwaka ujao,wakati alifunga goli la
pekee dhidi ya Uganda.
Bao hilo liliibuka kuwa bao muhimu sana kwa
Zambia kwa kuwa ilipoteza mechi iliyofuatia kwa bao moja kwa bila,
lakini ikafuzu kwa fainali za mwaka 2013 zitakazo andaliwa nchini Afrika
Kusini baada ya kushinda kwa magoli 9-8 kupitia mikwaju ya penalti.
Mikakati ya kufuzu kwa kombe la Dunia.
Na zaidi ya hayo yote, Katongo amechangua pakubwa harakati za kufufua matumaini ya Zambia ya kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia ya mwaka wa 2014.
Zambia ililazwa magoli 2-0 na Sudan mjini
Khartoum mwezi Juni, matokeo ambayo hadi wakati huu hayajathibitishwa,
huku uchunguzi ukiendelea kuhusu hatua ya Sudan ya kumshirikisha
mchezaji ambaye hakuwa amesajiliwa.
Wiki moja baada ya mechi hiyo Zambia ilichuana
na Ghana na Katongo kwa mara nyingine ndiye aliyefunga bao la ushindi na
hivyo kuimarisha matumaini yao ya kufuzu.
Ikiwa Christopher Katongo ataendelea na hali
aliyo nayo kwa sasa, huenda akaisaidia Zambia kuandikisha matokeo mazuri
wakati wa michuano ya kuwania kombe la dunia nchini itakayoandaliwa
nchini Brazil miezi kumi na minane ijayo.
0 comments:
Post a Comment