BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KENYA YAKUMBWA NA UVAMIZI, WAFUGAJI WAPORA MIFUGO ENEO LA BARAGOI.


Ramani ya Kenya

HABARI kutoka Kenya zinasema watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi wamevamia kijiji kimoja karibu na mji wa Baragoi, kaskazini magharibi mwa Kenya na kuiba mamia ya mifugo.

Majambazi hao karibu mia mbili wanasemekena kuwa na silaha nzito.

Watu wengi wameripotiwa kuhama eneo hilo.
Zaidi ya polisi arobaini waliuawa na wezi wa mifugo katika eneo hilo la Baragoi mwezi Novemba mwaka huu.

Bunge la Kenya, Ijumaa liliitaka serikali kuunda Tume ya uchunguzi kuhusu kuuawa kwa polisi, tukio baya kabisa kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: