BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

STARS YAILAZA ZAMBIA MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA KWA BAO 1-0 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.

Mchezaji wa Taifa Stars Hamis Mcha (7)akitafuta mbinu ya kuwatoka wachezaji wa Zambia maarufu kama Chipolopolo wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa wa kombe la Afrika jana.
Mshambuliaji wa Taifa Stars Mrisho Ngassa akimiliki mpira ambaye ndiye aliyeifungia Stars bao pekee katika mchezo huo.

TIMU ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeilaza timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo kwa bao moja kwa bila katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa katika uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam, Tanzania.

Katika mechi hiyo bao pekee la washindi, lilipatikana sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza likitiwa kimiani na mshambuliaji Mrisho Ngassa.

Timu ya Zambia, ambayo ni mabingwa wa Afrika ikiwa pia timu bora ya mwaka barani Afrika na yenye mchezaji bora wa mwaka wa BBC, Christopher Katongo, ilitawala mpira kipindi cha kwanza lakini ikokosa umakini katika umaliziaji.

Kwa upande wa timu ya Tanzania, ambao walionekana kutojiamini katika kipindi hicho, taratibu walibadilika, na kumiliki sehemu ya kiungo.

Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto,Frank Domayo na Salum Abubakar waliichosha ngome ya Zambia kwa kuelekeza mashambulizi mengi, langoni mwa Chipolopolo.
Mrisho Ngassa kama angekuwa makini zaidi angeweza kuipatia timu yake bao la mapema zaidi.

Timu ya Zambia ilichezesha nyota wake wengi akiwemo Christopher Katongo na Stopila Sunzu ambaye anatarajiwa kujiunga na timu ya Reading ya England.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: