Polisi wakielekeza watoto kuondoka katika shule ya msingi ya
Sandy Hook.
TAARIFA kutoka jimbo la kaskazinimashariki la Connecticut nchini marekani limesema watu 26 wengi wakiwa watoto wadogo wameuwawa katika shambulizi la pamoja la kupigwa risasi kwenye shule ya msingi.
Afisa wa Polisi katika jimbo hilo la Connecticut J. Paul Vance, aliwaambia waandishi wa habari kwamba shambulizi hilo limehusisha wanafunzi na wafanyakazi na kwamba mshambuliaji pia alikufa.
Afisa huyo hakueleza ripoti zaidi juu ya tukio hilo akisema kuwa umuhimu wa polisi hivi sasa ni kuwapa wazazi taarifa juu ya tukio hilo.
Afisa kutoka ofisi ya gavana amesema gavana alihuzunishwa juu ya tukio hilo na alikwenda kukutana na familia za wanafunzi.
Rais barack Obama ametoa wito kwa maafisa wa usalama huko Connecticut kuelezea kusikitishwa kwake na kuahidi kuwasaidia.
Tukio hilo limetoa ijumaa asubuhi katika shule ya msingi ya Sandy Hook Huko Newtown , Connecticut.
0 comments:
Post a Comment