BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIKOSI CHA YANGA KIKIWA KINAONDOKA KWENDA UTURUKI


 
Domayo & Msuva
Nizar Khalfani akiwa uwanja wa ndege

wachezaji wakisubirai muda wa ukaguzi
David Luhendee na Said Bahanuzi 
Nadir Haroub na Baraka Kizuguto
Kocha Mkuu Ernest Brandts akiwa na mjumbe wa kamatai ya utendaji ambaye pia ni mkuu wa msafara Mohamed Nyenge
 


 Ladislaus Mbogo akiwa na Nadir Haroub Canavaro Uwanja wa Ndege JK Nyerere
 —


Meneja wa timu Hafidh Saleh
 — in Dar es Salam.
Viongozi wa Yanga wakiwa uwanja wa ndege

 
YANGA SC, mabingwa mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wameondoka Alfajiri ya leo, saa 10:30 usiku kwenda  Uturuki kuweka kambi ya mazoezi ya wiki mbili.
Kikosi kizima cha Yanga kilikuwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere tangu saa 8:00 usiku kwa taratibu za kusafiri katika ziara hiyo Yanga itaweka kambi katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa Uturuki na itafikia katika hoteli ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Kikosi cha Yanga kilichoondoka Alfajiri ya leo ni makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.
Viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende wakati washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza.
Upande wa benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi Freddy Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na Maofisa wengine ni Daktari wa timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Nyenge.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: