MHANGA wa ubakaji na mauaji yaliyozusha maombolezo makali pamoja na
hasira nchini India amefanyiwa taratibu za mazishi kwa kaida za Kihindi,
kwa kuchomwa tukio lililofanyika kwa faragha leo Jumapili.
Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake mwenye umri wa miaka 23, ambaye alisababisha maandamano makubwa nchi nzima tangu aliposhambuliwa kinyama katika basi mjini New Delhi wiki mbili zilizopita, alichomwa moto bila kuwapo watu ambao wangeshuhudia tukio hilo kwa ombi la wazazi wake waliokuwa na fadhaa kubwa.
Mwili wa marehemu ukichukuliwa katika jeneza.
Taratibu hizo za mazishi za kuchoma moto , zilifanyika baada ya ndugu na marafiki kufanya taratibu za mwisho za maombi kwa muda mfupi katika wilaya ya kusini magharibi ya Dwarka mjini Delhi, kwa mujibu wa waombolezaji ambao wamemweleza msichana huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa taaluma ya udaktari kuwa alikuwa mtu anayetambulika na wengi na mwenye kipaji.
"Nimekuja kwa sababu nilikuwa nampenda kwa dhati msichana huyu.
Alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko wasichana wengine wote katika eneo tunakoishi," amesema Meena Rai, ambaye alikuwa rafiki wa karibu na jirani.
Waziri mkuu awataka Wahindi kuwa watulivu
Waziri mkuu Manmohan Singh na Sonia Gandhi, kiongozi wa chama kikuu tawala cha Congress, walikuwa katika uwanja wa ndege mjini New Delhi kuwapa pole wazazi wa msichana huyo wakati mwili wake ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwa ndege ya kukodi ikiwa na mwili wa mtoto wao.
Balozi wa India nchini Singapore T.C.A Raghavan katika hospitali ya Mount Elizabeth.
Lakini madaktari wameshindwa kuzuwia viungo vyake kadha vilivyoshindwa kufanyakazi na alitangazwa kuwa amefariki katika saa za alfajiri siku ya Jumamosi Dec 29/ 2012.
Kifo chake kilisababisha serikali kuahidi ulinzi bora zaidi kwa wanawake, na tathmini ya kina kwa taifa hilo ambapo matukio ya ubakaji hutokea kila siku na udhalilishaji huo wa kingono hupuuziwa kila mara, kama mchezo wa mzaha tu.
Msichana akishiriki katika maandamano India
Wimbi la maandamano lilizuka nchini India tangu shambulio hilo usiku wa
Desemba16 wakati mwanamke huyo alipofanyiwa unyama huo pamoja na
kushambuliwa kwa kupigwa kwa chuma, na kusababisha kupata majeraha
mabaya tumboni.Mishumaa yawashwa kumuenzi marehemu
Maelfu ya watu walishiriki katika tukio la kuwasha mishumaa usiku siku ya jumamosi baada ya waziri mkuu Singh kuongoza miito ya kuwataka watu kuwa watulivu na kuepusha kurejewa kwa maandamano yaliyokuwa na ghasia.
Wanafunzi na wanaharakati wakishiriki maandamano nchini India
Msichana huyo alitarajia kuolewa na mpenzi wake ambaye nae alijeruhiwa
katika shambulio hilo, amesema hayo Meena Rai , ambaye amekuwa akifanya
ununuzi kwa ajili ya maandalizi ya haurusi hiyo na marehemu. Harusi ilikuwa inatarajiwa kufanyika mwezi Februari mwaka ujao.
0 comments:
Post a Comment