LICHA ya vizuizi vya barabarani na kuwepo kwa wanajeshi wengi katika mji mkuu wa Misri Cairo , viongozi wa upinzani wanasema wataendelea kuweka msukumo kwa rais ili awezea kufuta kura ya maoni ya Jumamosi.
Muungano wa Upinzani wa National Salvation Front unaoongozwa na waliberali ikiwa ni pamoja na Mohamed Elbaradei na Amr Mousa wamewataka wafuasi wao kuandamana kuelekea jumba la rais huko Cairo Jumanne.
Maandamano dhidi ya rais Morsi.
Katika taarifa Jumapili usiku rais Mohamed Morsi aliyekataa kurudi nyuma, Jumatatu alilipa jeshi mamlaka ya kukamata raia ikiwa kama sehemu ya amri ya kusaidia kuleta usalama kwa ajili ya kura ya maoni.
Amri hiyo inawapa kazi wanajeshi kusaidia Polisi kulinda taasisi muhimu.
0 comments:
Post a Comment