BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Mama Salma Kikwete Awaandalia 'Menu' Watoto Yatima



Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,(WAMA,) akiwapungia mkono watoto yatima (hawapo pichani) walihudhuria sherehe ya mwisho wa mwaka iliyofanyika kwenye viwanja vya Taasisi hiyo karibu na Ikulu jijini Dar tarehe 8.12.2012.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na mtoto mlemavu wa ngozi aliyekuwa miongoni mwa watoto yatima walioalikwa kwenye sherehe ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na taasisi yake kwa kushirikiana na Kampuni ya Saruji ya Twiga na Dar North Rotary Club kutoka vituo vya Malaika Orphan Centre (Mkuranga), Mwandaliwa Islamic Orphan Centre (Boko), Umra Orphan Centre (Magomeni), Kurasini National Orphan Centre na Mama Lenga (Kigogo).
 Mke wa Rais na Mweyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga Bwana Pascal Lesoinne kugawa zawadi mbalimbali kwa watoto yatima wanaolelewa katika baadhi ya vituo vya Dar es Salaam katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi za WAMA tarehe 8.12.2012.
 Baadhi ya watoto yatima wakipata chakula cha mchana walichoandaliwa na Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Twiga Cement Bwana Pascal Lesoinne mara baada ya sherehe ya mwisho wa mwaka waliyowaandalia watoto yatima kwenye ofisi za WAMA tarehe 8.12.2012.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: