Wafuasi wa Lema wakishangilia barabarani wakati Mbunge huyo akipita.
Mbwembwe za waendesha pikipiki wengine ziliwashinda na kuanza kuanguaka jambo ambalo ni hatari.
Furaha hiyo ilikuwa kwa kila aliye Mwanachadema.
Mke wa Mbunge Godbless Lema akiwa kwenye gari pamoja na mtoto wao wakati wa mapokezi hayo.
Lema Arusha anafananishwa na Rais Barack Obama
Furaha ya namna hii ya kupita kikomo inaweza kusababisha watu kupoteza maisha endapo ajali inaweza kutoka kwani ni uvunjaji wa sheria za usalama barabara kama wanavyooneka vinaja hawa wakining'inia katika daladala bila hofu.
MAPOKEZI
ya Kihistoria katika jiji la Arusha yamefanyika leo wakati wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA),wakimpokea Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.
Makundi makubwa ya wanachama hao na wafuasi walimiminika kwa wingi kuanzia Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hadi katika Viwanja vya
Kilombero mjini hapa.
Mapokezi
hayo yamefanyika wakati Godbless Lema alipokuwa akirejea mjini Arusha
akitokea jijini Dar es Salaam kusikiliza hukumu ya Rufani ya Keshi yake
ya Kuvuliwa Ubunge iliyotolewa maamuzi ya kumrtejeshea Ubunge wake
Desemba 21,2012.
Maelfu
ya wananchi wakiwa katika msafara mrefu zaidi ya pikipiki 500 na magari
ulianzia Uwanja wa Ndege KIA mara baada ya Mbunge huyo kuwasili
uwanjanai hapo majira ya saa 4:20 Asubuhi
0 comments:
Post a Comment