Wanavijiji wakiangalia maiti kufuatia mapambano ya kikabila huko Kipao.
MAAFISA wa serikali nchini Kenya wanasema watu wasiopungua 39, wanavijiji 30 na washambuliaji tisa wameuwawa katika mapambano mengine mapya kati ya makundi mawili hasimu ya kikabila katika mkoa wa kusini mashariki wa Tana River.
Ofisa mmoja wa polisi katika eneo anasema kundi la kabila la Pokomo lililokuwa limebeba mishale na bunduki lilivamia kijiji cha watu wa Orma, alfajiri ya Ijumaa.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya linasema watoto 13 na wanawake sita walikuwa miongoni mwa waliouwawa katika shambulizi kwenye kijiji cha Kipao. Inasema kiasi cha nyumba 45 zilichomwa moto.
Polisi wanasema wanafahamu mahali washambuliaji wanakotoka na wanawafuatilia.
Makundi hayo mawili yamefanya mifululizo ya mashambulizi ya mauaji na mashambulizi mengine kama sehemu ya mgogoro unaoendelea juu ya ardhi na maji.
Mwezi wa Agosti na Septemba zaidi ya watu 100 waliuwawa katika mapambano kati ya kabila la Pokomo ambayo ni jamii kubwa ya wakulima na kabila la Orma ambalo linafahamika kwa ufugaji.
Umoja wa Mataifa unasema baadhi ya mauaji huenda yanahusiana na kuongezeka kwa mivutano kuhusu uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Zaidi ya watu 1,100 waliuwawa katika ghasia za uchaguzi mkuu uliopita nchini Kenya wa mwaka 2007.
0 comments:
Post a Comment