Kwa ufupi
Kitendo cha kuagiza nguzo nje ni matumizi mabaya ya
fedha za umma, kwani kinaongeza gharama za bidhaa hiyo hapa nchini na
kuua viwanda vya ndani.
Nyaya za umeme.
SERIKALI imepiga marufuku Shirika la Umeme Tanzania (Tanaesco) kununua nguzo za umeme kutoa nje ya nchi.
Katika marufuku hiyo, imeeleza kuwa kitendo cha
kutoa tenda kwa kampuni za nje na kuacha za ndani ya nchi zinazozalisha
nguzo hizo ni cha aibu kwa taifa.
Akizungumza baada ya kufanya ziara ya siku moja ya
kikazi, Naibu Waziri wa Nishari na Madini, George Simbachawene alisema
kuanzia sasa nguzo za umeme hazitaagizwa kutoka nje kutokana na viwanda
vya ndani kuzalisha nguzo zinazotosheleza.
Alisema kitendo cha kuagiza nguzo nje ni matumizi
mabaya ya fedha za umma, kwani kinaongeza gharama za bidhaa hiyo hapa
nchini na kuua viwanda vya ndani.
Alisema kimsingi Tanzania ilistahili kuuza nguzo nje ya nchi na si kununua na kwamba kitendo hicho kinaingizia Serikali na wananchi wake harasa kubwa.
Alisema kimsingi Tanzania ilistahili kuuza nguzo nje ya nchi na si kununua na kwamba kitendo hicho kinaingizia Serikali na wananchi wake harasa kubwa.
Waziri huyo alitoa kauli hiyo baada ya viongozi wa
viwanda vya kuzalisha nguzo za umeme vya Green Resouces na Sheda
General Suplies LTD vyote vya wilayani Mufundi mkoani hapa kueleza kuwa
kampuni zinazouza nguzo hapa nchini zimekuwa zikinunua nguzo toka
katika viwanda vyao.
Imeelezwa kuwa nguzo zinazotumiwa na shirika hilo huagizwa kutoka nje ya nchi ikiwamo Kenya na Afrika ya Kusini kwa madai kuwa nguzo za hapa nchini hazina ubora na hazitoshelezi.
Imeelezwa kuwa nguzo zinazotumiwa na shirika hilo huagizwa kutoka nje ya nchi ikiwamo Kenya na Afrika ya Kusini kwa madai kuwa nguzo za hapa nchini hazina ubora na hazitoshelezi.
0 comments:
Post a Comment