WANAWAKE nchini Swaziland wako katika hatari ya
kukamatwa na polisi iwapo watavaa sketi fupi au blauzi ambazo
zitaonyesha tumbo likiwa wazi.
Msemaji wa polisi Wendy Hleta amesema polisi
watatekeleza sheria ya mwaka1889 ambayo inapiga marufuku uvaaji wa nguo
zinazokosa maadili.
Msemaji huyo wa polisi pia amesema wanawake wanaovaa nguo fupi ni kivutio cha wabakaji.
Hata hivyo, sheria hiyo ya kikoloni haitumiki
katika uvaaji wa nguo za kijadi ambazo zinavaliwa na wanawake, sehemu
kubwa ya miili yao inaachwa wazi.
Mavazi hayo huvaliwa wakati wa sherehe, zikiwemo za mwaka zinazompa Mfalme fursa ya kuchagua mke wake mpya.
Mwaka 2000, serikali ilitunga sheria inayowataka
wanafunzi wa kike kuanzia miaka 10 na zaidi kuvaa sketi zinazovuka
magoti kama njia ya kuwalinda dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Swaziland ina idadi ya watu milioni1.2 na moja kati ya nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya ukimwi duniani.
Bi Hleta amesema sheria hiyo ya mwaka1889 haijaweza kutekelezwa katika miaka ya karibuni.
Amesema polisi wanataka kuwajulisha wanawake kuwa sheria hiyo bado ipo na inafanya kazi.
Baadhi ya wanaume katika mji wa Manzini wamesemekana kuwalalamikia wanawake wanaovaa kuvaa nguo fupi.
0 comments:
Post a Comment