MJUMBE wa amani wa kimataifa Lakhdar Brahimi leo anatazamiwa kuanza
mazungumzo na Rais Bashar al Assad wa Syria mjini Damascus wakati
mapigano makali yakiendelea katika maeneo kadhaa ya mji mkuu huo.
Kuwasili kwa mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu kunakuja wakati shambulio la anga la vikosi vya serikali kwenye duka la mikate katika mji wa kati wa Halfaya limeuwa takriban watu 109 wakati wengine zaidi ya hamsini wako katika hali mahututi.
Iwapo litathibitishwa shambulio hilo katika mji huo wa Halfaya katikati ya Syria, uliotekwa na waasi wiki iliopita, litakuwa mojawapo ya shambulio la anga lililosababisha maafa makubwa kabisa katika mzozo huo wa Syria. Hali ilikuwa ya taharuki kufuatia shambulio hilo.
Shambulio lasababisha maafa makubwa
Duka la mikate baada ya kushambuliwa na ndege za Syria.
Kwa mujibu wa mwanaharakati mmoja katika mji huo, Samer al- Hamawi, ameshuhudia mrundiko wa maiti ukiwa barabarani wakiwemo wanawake na watoto.
Uasi nchini Syria umegeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo idadi ya vifo kwa siku hufikia mia moja wakati jeshi la nchi hiyo likiwashambulia waasi ambao wamefanikiwa kuteka maeneo kadhaa nchini humo na kusonga mbele kwenye mapambano kukaribia mji mkuu wa Damascus.
Kwa mujibu wa Shirika la Kuangalia Hali Haki za Binaadamu nchini Syria zaidi ya Wasyria 180 wakiwemo raia na wapiganaji wameuwawa hapo jana.
Suala la kumpindua Assad lisahaulike
Rais Bashar al-Assad wa Syria.
Amesema anatowa ushauri wa jumla kwa vikundi vya kisiasa ambavyo vinakataa mazungunmzo kwamba muda unayoyoma.
Na wachapuke kuchukuwa hatua ya kutafuta suluhisho la kisiasa. Ameongeza kusema kwamba " Harakati za kijeshi za kujaribu kuiangusha serikali au kumundowa rais au kuutwaa mji mkuu.Jambo hilo msahao!"
Kauli yake hiyo alioitowa kwenye mkutano na waandsihi wa habari mjini Damascus inaonekana kwenda kinyume kabisa na ile iliyotolewa na makamo wa rais wa Syria wiki iliopita ya kupendelea suluhu ambapo amesema hakuna mtu atakayeshinda katika vita hivyo na kutowa wito wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.
Mataifa ya magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu zimekuwa zikisisitiza kwamba Assad lazima ajiuzulu.
0 comments:
Post a Comment