Mkutano wa chama cha upinzani cha Chadema kumaliza kampeni za uchaguzi wa 2010 Dar es Salaam.
VYMA vya siasa pamoja na taasisi za haki za binadamu nchini Tanzania vimeelezea wasiwasi wake juu ya matukio ya mauaji ya raia na askari polisi yanayoripotiwa kutokea katika sehemu mbalimbali nchini katika siku za hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurungezi mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt Helen Kijo-Simba ametaka serikali na mamlaka husika kuchukulia mauaji hayo hasa ya askari polisi kwa uzito wa kipekee kwani yana athari kubwa katika mustakabali wa amani na utulivu wa nchi.
Mkurugenzi huyo wa kituo cha sheria na haki za binadamu amesema matukio mengi ya mauaji nchini Tanzania yameongezeka zaidi kwa mwaka huu wa 2012 pengine kutokana pia na kuwepo tatizo katika kufuata utawala wa sheria kwa waliopewa mamlaka ya kusimamia usalama na amani ya nchi.
Dakta Bisimba alikuwa akizungumzia matukio mbalimbali ikiwemo mauaji ya askari polisi wawili yaliyofanywa na raia huko Ngara mkoani Kagera , mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoani Mwanza marehemu Lebaratus barlow na pia mauaji ya askari wa kikosi cha polisi cha kutuliza ghasia huko visiwani Zanzibar na mauaji mengine ya raia wa kawaida katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika mikusanyiko ya kisiasa, iliyosabaisha pia kuuwawa kwa mwandishi wa habari daudi mwangosi.
Wakati wanaharakati wa haki za binadamu wakitaka hatua hizo dhidi ya mauaji ya raia, chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika moja ya maazimio yake yaliyotokana na kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichoketi hivi karibuni jijini Dar es salaam, kimetaka rais Jakaya Kikwete kuchukau hatua dhidi ya mapendekezo waliyoyatoa ya kutaka aunde mahakama ya kikatiba kushughulikia mauaji ya raia.
Mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumanne, kuzungumzia maazimio ya kamati kuu ya chama hicho pamoja na masuala mengine amesema wanadhani serikai haifanyi vya kutosha kukabili mauaji ya raia katika maeneo mbalimbali nchini..
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa taifa wa CHADEMA amewaeleza wanahabari kuwa kamati kuu ya chama hicho imeazimia kutumia njia mbalimbali ikiwemo ya kibunge kupitia hoja binafsi kuwasilisha bungeni mapendekezo ya marekebisho ya katiba ya mpito kuhakikisha tume huru ya uchaguzi na sheria za uchaguzi zinafanyiwa marekebisho kabla ya katiba mpya ili uchaguzi wa 2015 ufanyike kwa haki..
CHADEMA imeishutumu serikali na tume ya taifa ya uchaguzi kukwepa wajibu wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura toka mwaka 2010 hali itakayoathiri haki ya kikatiba ya wananchi kupiga kura na matokeo ya chaguzi za marudio zinazofanyika ambapo wanataka 2013 daftari hilo lifanyiwe marekebisho ili pia litumike katika kura za maoni za katiba mpya.
0 comments:
Post a Comment