Mbunge
Filikunjombe (kushoto) akimchana diwani wa kata ya Madope Bw Mhagama
(kulia) katikati ni mwenyekiti wa CCM wilaya Bw Kolimba akisikiliza
kwa umakini
KATIKA hali isiyotegemewa mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani
Njombe Deo Filikunjombe (CCM) amemkataa mbele ya viongozi wa CCM
na wapiga kura diwani wa kata ya Madope jimbo la Ludewa kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Godfrid Mhagama kwa madai kuwa ni diwani
anayeongoza kwa kumdanganya yeye kama mbunge pamoja
na wapiga kura wa kata hiyo.
Mbunge Filikunjombe alisema kuwa diwani huyo amekuwa
ni mmoja kati ya watu wanaoeneza chuki ya ukabira katika
kata hiyo kwa kuwabeza viongozi wa wilaya na mbunge kutokana na
kuwa si wenyeji wa kata hiyo ni watu kutoka ukanda wa ziwani jambo
ambalo ni hatari kwa maendeleo ya kata hiyo iwapo siasa za ukabira
na ukanda zitapewa nafasi.
Akizungumza
katika mkutano maalum kijijini hapa mara baada ya kufunguza ofisi
ya chama cha ushirika wa kuweka na kukopa ya Farasa Saccos ,juzi
Filikunjombe alisema kuwa moja kati ya kata ambazo
madiwani wake toka walipochaguliwa mwaka 2010 hawafanyi kazi ya
kimaendeleo na badala yake wamekuwa wakieneza chuki
ya kuwagawa viongozi na wananchi ni pamoja na kata hiyo ya Madope
ambapo diwani amekuwa akiendesha majungu mitaani na kuacha kusimamia
shughuli za kimaendeleo.
Alisema kuwa diwani
huyo amekuwa ni kikwazo kikubwa ndani ya CCM kutokana
na kushindwa kusimamia ujenzi wa shule ya Msingi Mangalanyena
,kushindwa kusimamia ujenzi wa Zahanati katika kijiji hicho pamoja na
ujenzi wa barabara na kila anapoulizwa amekuwa akitoa majibu ya uongo
mbele yake .
Mbunge huyo
alisema katika hali ya kushangaza diwani huyo baada
ya kuulizwa mkakati wa kata katika kusimamia ujenzi wa Zanahati ya
kata kijijini hapo alieleza kuwa mkakati wa ujenzi huo na
miradi mingine iliyosimama katika kata yake ya Madope imeingizwa
katika kipindi cha fedha cha mwaka 2013 /2014 bajeti huku
akitambua kuwa huo ni uongo kwani bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/2014
bado kupitishwa.
Hata hivyo alisema
kupitia diwani huyo kata hiyo wamekuwa wakiwachukia viongozi wa
chama na serikali ambao si wa kabila la kwao
huku wakiendelea kukwamisha miradi ya maendeleo katika kata hiyo kama
njia ya kuwafanya wananchi waungane nao
katika kuwachukia viongozi wa wilaya hiyo .
“Nimechukizwa sana
na tabia ya mheshimiwa diwani wa kata hii Bw Mhagama
kwa kushindwa kufanya kazi za kimaendeleo badala yake anashinda vijiweni kuwaelewa wananchi uongo juu ya viongozi
kuwa si wa ukanda wao …..nasema diwani kama unataka
kuendelea kuendesha uongo na kushindwa kufanya kazi yako ni vema
ukakaa pembeni ili wananchi waendelee kujiletea maendeleo….nchi yetu
na chama chetu hatuchaguani kwa ukabila wala rangi tunachangana kwa
uwezo wa mtu na utendaji sio hivyo unavyofanya wewe”huku akishangiliwa
na wananchi waliofika katika mkutano huo
Filikunjombe
aliwataka wananchi kutomsikiliza diwani huyo iwapo
atashindwa kubadilika na kuendelea kueneza chuki katika kata hiyo
kati ya viongozi wa juu wa wilaya na jimbo na wananchi wake .
Wakati
kwa upande wake diwani Mhagama alipofuatwa na mwandishi wa habari
hizi ili kujibu tuhuma hizo dhidi yake alisema kuwa si kweli kama
amekuwa akieneza siasa za ukabila katika kata hiyo na kuwa
wanaofanya hivyo ni watu baki na sio yeye kama ambavyo mbunge amekuwa
akimtuhumu .
Kuhusu kukwama
kwa miradi ya kimaendeleo katika kata yake ya Madope
alisema kuwa kutokana na maelekezo ya mbunge atahakikisha anakuwa
mbele katika kusimamia miradi hiyo na kuwa kwa upande wake amekuwa
akikwamishwa na watendaji wa Halmashauri
ambao wamekuwa hawafiki kufanya ukaguzi wa miradi katika kata hiyo.
Katika hatu nyingine mbunge Filikunjombe ameahidi kusimamia
ujenzi wa zahanati hiyo hadi ukakapokamilika
ili kuwawezesha wananchi hao wa kupata huduma ya afya jirani zaidi.
0 comments:
Post a Comment