JUMLA ya Sh bilioni 2.7, zimetengwa na Serikali, kwa ajili ya kuwalipa
fidia wafanyabiashara 120 wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo.
Akizungumza na wadau wa biashara jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam,
Didas Masaburi, alisema hadi sasa zaidi ya wafanyabiashara 100 wamelipwa
Sh bilioni 2.2, kwa ajili ya kupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Alisema lengo la kuwaondoa wafanyabiashara hao, ni kupisha mradi wa
mabasi yaendayo kasi, ambayo yanalenga kumaliza tatizo sugu la foleni.
Alisema
mradi huo wa Dart, ulitakiwa kukamilika mwaka jana, lakini
ulishindikana kutokana na ulipaji wa fidia kwa wafanyabiashara waliopo
katika kituo hicho kushindikana.
“Tatizo kubwa la kushindwa
kukamilika kwa mradi huu, ni kituo cha mabasi hadi leo (jana),
mkandarasi hajaanza kazi, ipo haja kwa wafanyabiashara kukubali hasara
ili kufanikisha mradi huo uendelee.
“Mradi huu, utajengwa na
mkandarasi kutoka kampuni ya Beijing Constraction, kwa msaada wa Benki
ya Dunia ambao unatakiwa kukamilika mwaka 2014/15, kama utashindwa
kukamilika mradi utasogezwa mbele au kufutwa kabisa.
“Ni jambo la
aibu kwa nchi yetu ya Tanzania, kushindwa kukamilisha mradi huu, kwani
katika nchi za wenzetu tayari umeshakamilika mradi huu wa Dart,” alisema
Masaburi.
Alisema kutokana na kuchelewa, ipo haja kwa
wafanyabiashara hao kuhama kwa hiari yao kabla ya Desemba 30, mwaka huu
ili kupisha shughuli kwa mkandarasi kuanza kufanya kazi yake.
Alisema iwapo watashindwa kuhama mpaka Januari mosi, 2013 watatumia nguvu ya Serikali kuvunja maeneo yote.
Alisema
mradi wa mabasi yaendayo kasi, yana faida kubwa kwa wananchi wa Jiji la
Dar es Salaam, kwani jumla ya vijana 3,000 watapatiwa mafunzo na
wengine kupata ajira.
Alisema jumla ya mabasi 700 ya daladala
yataondoshwa kwa ajili ya kuepuka msongamano na kupisha mradi huo ambao
utaleta heshima kubwa katika Jiji la Dar es Salaam .
Aliwataka wamiliki wa daladala, kuachana na mabasi hayo na badala yake waanze kununua mabasi makubwa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment