BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKURUGENZI MKUU BENKI YA NBC AJIUZURLU

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lawrence Mafuru, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa huo. Uamuzi wa Mafuru, umekuja miezi michache tangu Bodi ya Benki hiyo kutangaza Oktoba 7, mwaka huu kumrudisha kazini, baada ya kusimamishwa kwa zaidi ya mwezi.

Mafuru alisimamishwa ili kupisha uchunguzi dhidi yake juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi yake zilizokuwa zikimkabili.

Mafuru alisimamishwa Julai 19, 2012 na Bodi ya Wakurugenzi ya NBC, baada ya bodi hiyo kupokea malalamiko ya wafanyakazi kuhusu kuwapo ukiukwaji wa taratibu za kiutendaji ndani ya benki hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Mafuru alisema ameandika barua ya kujiuzulu ambayo aliiwasilisha kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBC jana.

Alisema hatua ya kujiuzulu kwake si hatua rahisi kwake, bali anapisha watu wengine wenye uwezo waweze kufanya kazi hiyo.

“Barua yangu kwa mwenyekiti wangu wa bodi, ni kwamba si uamuzi rahisi kufanya jambo kama hili na katika maisha yetu ya kazi mtu hufikia kuchukua maamuzi magumu kwa ajili ya maslahi ya jambo fulani.

“Uamuzi wa kuachia nafasi yangu ya kazi hii, unakwenda sambamba na malengo yangu ya kazi. Baada ya miaka minne ya kazi kubwa ya kimaendeleo katika NBC.

“Nilianza kwa nafasi kama mweka hazina tangu Agosti 2007 na baadaye kama Afisa Mkuu Mtendaji kuanzia Juni 2010 hadi sasa, nadhani kwamba ni sahihi kutafuta changamoto nyingine mahali pengine na kuruhusu wengine ili waendeshe meli ya NBC.

“Nikiangalia kazi ya miaka minne iliyopita, imekuwa ya kuridhisha sana na ya mafanikio makubwa, niliweza kusukumwa na ajenda ya mabadiliko ya shughuli za NBC. Sasa NBC imekuwa na nafasi kubwa na nzuri ya mizania.

“Tumejenga nguvu ya wafanyakazi wetu, wake kwa waume sambamba na kuboresha huduma bora kwa wateja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.

“Mbali na hatua hii, bado tumeweza kujiimarisha kiuchumi katika miaka mitatu ijayo sambamba na kukua na kuwaendeleza wafanyakazi wetu kitaaluma.

“Binafsi ninaishukuru bodi ya NBC, wenzangu katika timu ya usimamizi na wafanyakazi wote wa NBC kwa msaada na mabadiliko. Sina shaka katika akili yangu pamoja na uongozi mpya, wataimarisha mafanikio ambayo tumekuwa nayo katika kazi yetu ya kuleta mageuzi na kuwa benki ya ngazi ya pili nchini.

“Mafanikio haya yote, yasingewezekana kama nisingepata msaada kutoka kwa wafanyakazi wenzengu, wateja na wadau wengine ambao mimi napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwao.

“Ninaamini kutangaza kwangu kujiuzulu hakika ni njia ya safari ya mafanikio na kupitia familia yangu na mimi nafikiria wanastahili, kuanza msimu wa sherehe, ambayo mimi ninawatakia kazi njema na kusameheana pale tulipokoseana katika maisha yangu, wakati nilipokuwa NBC,” alisema Mafuru katika barua yake ya kujiuzulu, ambayo MTANZANIA imefanikiwa kupata nakala.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: