MKUTANO wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi jana
Jumamosi jan umerefusha uhai wa mkataba wa Kyoto, ambao ndio pekee
unaolazimisha mataifa kupunguza utoaji wa gesi chafu, ukiwa ushindi mdogo
na muhimu.
Ilichukua majadiliano marefu na saa kadha bila kupata usingizi katika
mji mkuu wa Qatar, Doha hadi yalipofikiwa makubaliano kuhusu hatua za
mpito kuzuwia mabadiliko ya tabia nchi, yakisubiriwa makubaliano mapya
ya dunia ambayo yataanza kufanyakazi mwaka 2020.
Urefushwaji wa mkataba wa Kyoto uliidhinishwa hatimaye na mataifa ya
umoja wa Ulaya, Australia, Uswisi na mataifa manane mengine yenye
utajiri mkubwa wa viwanda yakitia saini upunguzaji wa lazima wa utoaji
wa gesi za viwandani ifikapo mwaka 2020.
Mataifa hayo yanawakilisha utoaji wa asilimia 15 wa gesi chafu
zinazoharibu mazingira duniani.
Kiongozi wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon
ameyakaribisha makubaliano hayo, ambayo yanatambulika kama lango la
Doha katika mazingira, kuwa ni hatua ya kwanza muhimu lakini amesema kwa
kupitia msemaji wake kuwa , "hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa."
Maandamano hayakukosa mjini Doha.
Mataifa tajiri yabanwa
Makubaliano hayo yanayafunga tu mataifa yaliyoendelea, yakiweka kando
mataifa makubwa yanayoendelea yanayochafua zaidi mazingira kama vile
China na India, pamoja na Marekani ambayo inakataa kuidhinisha mkataba
wa Kyoto.
Kimsingi, wataalamu wamesema kuwa kurefushwa kwa mkataba huo kutaleta
tofauti kidogo tu kwa viwango vya uchafuzi wa mazingira kwa kuwa
unajumuisha sehemu ndogo ya utoaji wa gesi hizo chafu na mataifa
yaliyotia saini yana malengo yake yaliyopitishwa kisheria hata hivyo.
"Ni hatua ndogo lakini muhimu kuelekea mbele," kamishna wa masuala ya
mazingira wa umoja wa Ulaya Connie Hegegaard amesema mwishoni mwa
mazungumzo hayo ambayo yaliendelea siku nzima ya Ijumaa hadi usiku na
kuingia katika siku nzima ya muda wa nyongeza, wakati nchi tajiri na
masikini zikipambana kuhusiana na utoaji wa fedha na fidia kwa ajili ya
madhara yaliyopatikana kwa mazingira.
Baada ya siku 12 za mvutano ambao ulionekana kushindwa tangu mwanzoni,
mwenyekiti wa mkutano huo Abdullah bin Hamad al-Attiyah hatimaye
aliharakisha kupitishwa kwa makubaliano hayo jioni ya
Jumamosi(08.12.2012).
Rais wa mkutano huo wa umoja wa mataifa Abdullah bin Hamad Al-Attiyah.
Hapo kabla aliwahimiza wajumbe kupata muafaka na "sio kuanzisha
majadiliano ambayo hayana mwisho tena kwa sababu hatutamaliza", onyo
ambalo hata hivyo lilipuuziwa.
Atumia rungu
Attiyah alilazimika kusubiri katika ukumbi kwa zaidi ya saa nne wakati
mapambano yakiendelea.
Makamu waziri mkuu huyo alizuwia mapambano zaidi
kutokana na kupinga kwa baadhi ya mataifa wakati akipiga rungu lake kila
mara na huku akitoa tamko: "Imeamuliwa hivi" huku akishangiliwa kwa
nguvu.
Urusi ilitoa pingamizi la kupitishwa kwa makubaliano ya Kyoto, ambayo awamu yake ya kwanza inamalizika Desemba 31.
Duru ya hivi sasa ya mazungumzo ya mabadiliko ya tabia nchi ya Umoja wa
Mataifa, ambayo imeonekana kuburuza miguu mno wakati wajumbe wa
majadiliano wakibishana hadi dakika za mwisho kama vile katika mchezo wa
karata na kujaribu kuvicha karata zao, wakishindwa kupata uvumbuzi
kuhusu utoaji wa fedha pamoja na mikopo ya hewa chafu.
Biashara ya gesi chafu
Hewa chafu ina maana ya biashara ya utoaji wa gesi zinazoharibu
mazingira, viwango ambavyo nchi ziliruhusiwa kutoa katika mkataba wa
Kyoto wa mwaka 1997 na havikufikiwa, ikiwa ni kiasi cha tani bilioni 13
za gesi hizo kwa jumla.
Poland na Urusi bado zina kiwango hicho cha mkopo, kwa kuwa zilitoa gesi
chafu cache zaidi kuliko viwango inavyoruhusiwa, na zinasisitiza kuwa
ziruhusiwe kuhifadhi tofauti iliyopo kupindukia mwaka 2012, hatua ambayo
makundi mengine yanapinga kwa nguvu zote.
Waziri wa mazingira wa Poland Marcin Korole.
Makubaliano hayo hayaruhusu mikopo ihifadhiwe, lakini masoko muhimu,
ikiwa ni pamoja na umoja wa Ulaya , Australia na Japan , imeelezwa
katika waraka huo kuwa hazitaruhusiwa kununua.
Mataifa yaliyoendelea yalikuwa katika mbinyo mjini Doha kuonyesha vipi
yanataka kuweka ahadi yao ya kuongeza fedha kwa ajili ya mazingira kwa
nchi masikini kufikia dola bilioni 100 kila mwaka ifikapo mwaka 2020,
kutoka idadi ya jumla ya dola bilioni 30 katika mwaka 2010 hadi 2012.
0 comments:
Post a Comment