Kwa ufupi:
“Wenye vipato vya chini hawawezi kusoma katika shule
hizi kwa sababu zinatoza ada kubwa ambayo maskini hawezi kumudu gharama
zake,” alisema.
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema elimu inayotolewa nchini ni ya kibaguzi.
Kardinali Pengo alisema hayo Dar es Salaam jana
alipokuwa akiwasilisha ujumbe wa maaskofu wa Kanisa Katoliki walioutoa
katika mkutano wao uliofanyika Oktoba 7 hadi 28, mwaka huu huko Roma,
Italia.
Alisema watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii wanapaswa kutoa kipaumbele katika upatikanaji wa elimu bora kwa kila Mtanzania.
Kardinali Pengo alisema hapendezwi na namna elimu
inavyotolewa nchini kwani kimfumo, baadhi ya shule zimekuwa
vitegauchumi, hivyo kuwa kikwazo kwa watu wenye kipato cha chini.
“Wenye vipato vya chini hawawezi kusoma katika
shule hizi kwa sababu zinatoza ada kubwa ambayo maskini hawezi kumudu
gharama zake,” alisema.
Askofu Pengo alionya kuwa endapo hali hiyo
itaachiwa, inaweza kuwafanya wale waliokosa elimu kuwa chanzo cha vurugu
kwa kuwa watasimama kidete kudai haki yao.
Maoni ya Katiba.
Katika hatua nyingine, Kardinali Pengo alizungumzia mchakato wa Maoni ya Katiba unaoendelea nchini, huku akiwaonya baadhi ya wanasiasa na taasisi mbalimbali za dini kuacha kuwashinikiza wananchi kutoa maoni kwa ajili ya masilahi yao binafsi.

“Kila mtu aruhusiwe kutoa maoni yake, lakini
lazima tukubaliane kuwa kila mtu ana maoni yake na maoni yote hayawezi
kuingizwa katika Katiba Mpya,” alisema Pengo.
Alisema kwa kuwa Katiba inagusa masilahi ya nchi,
ni vyema kila mwananchi akatumia fursa yake ya kuwasilisha maoni yake
mwenyewe.
Alitahadharisha kuwa wananchi wasiposhirikishwa
katika mchakato wa Katiba Mpya, wanaweza kuja kuikataa kwa sababu maoni
yao hayakuzingatiwa.
Suala la udini.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ameitaka Serikali kuchukua hatua za makusudi kwa wale wote watakaobainika kusababisha uharibifu wa mali za dhehebu la dini yoyote hapa nchini, kama wanavyofanya pindi kunapotokea uhalifu katika benki au wizi katika maeneo ya viongozi na sehemu nyingine.

Alisema nchi imegawanyika katika madhehebu
mbalimbali, hivyo inapotokea dhehebu moja kulitukana na kuharibu mali za
jingine, Serikali haipaswi kukaa kimya.
0 comments:
Post a Comment