Kwa ufupi:
Wakizungumza na Mwananchi jana, abiria hao walisema
kumekuwa na tatizo la kutotabirika kwa nauli za baadhi ya mabasi na hasa
katika kipindi hiki cha sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
BAADHI ya abiria wa mabasi wanaosafiri kwenda katika mikoa
mbalimbali wakitokea mkoani Mbeya, wameiomba Mamlaka ya Udhibiti wa
Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra), kuwashinikiza wamiliki wa
mabasi, kubandika kwenye mbao za matangazo, orodha za nauli halali za
safari, ili kudhibiti mchezo mchafu wa kuwabambikia watu nauli.
Vitendo hivyo, vimekuwa vikifanywa na wapigadebe
wa mabasi mbalimbali katika kituo kikuu cha mabasi cha jijini Mbeya na
hata katika miji mingine nchini.
Wakizungumza na Mwananchi jana, abiria hao
walisema kumekuwa na tatizo la kutotabirika kwa nauli za baadhi ya
mabasi na hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
Walisema wapigadebe katika mabasi hayo, wamekuwa wakiwabambikia watu nauli wasizostahili kulipa, jambo ambalo ni la kuwaumiza.
Abiria hao walisema kwa msingi huo, kuna haja kwa
Sumatra, kuwashinikiza wamiliki wa mabasi kuhakikisha kuwa wanabandika
kwenye mbao za matangazo katika ofisi zao, orodha za nauli halali.
“Hii itasaidia sana kuwafanya abiria kuachana na tatizo la wapigadebe kuwarubuni nauli,”alisema Johnson Abraham.
Abraham alisema ni jukumu la wamiliki wa mabasi ya
safari ndefu, kudhibiti tatizo hilo linaloelekea kuota mizizi kila
inapofika mwishoni mwa mwaka.
Abiria hao pia waliliomba Jeshi la Polisi,
kuwaondoa wapigadebe katika kituo kikuu cha mabasi, kwa maelezo kuwa
wamekuwa kero kubwa.
Walisema pamoja ma mambo mengine, watu hao wamekuwa wakitoa lugha chafu kwa abiria na hata kuwaibia mali zao..
“Wamiliki wa mabasi, wanapaswa kuwa na vijana wao
wanaotambulika kisheria, ili kuondokana na adha ya abiria ya kusumbuliwa
na wapigadeba.
Hali hiyo imekuwa ikichangia hata kuibiwa mali zao zikiwemo simu za mkononi,” alisema abiria mwingine.
Hali hiyo imekuwa ikichangia hata kuibiwa mali zao zikiwemo simu za mkononi,” alisema abiria mwingine.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Athuman Diwani,
alisema amepokea malalamiko hayo na kwamba wamewasiliana na Sumatra, ili
kuangalia namna ya kukabiliana na tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment